Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Hukumu ya Fitnah ( An-Namiymah )

Assallaam  Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Maana ya An-Namiymah Ni kufitinisha, kwa maana kuchongeza kwa kuhamisha au kupeleka maneno baina ya watu ili kusababisha wachukiane. Mfano kumwambia mwenzio: "Fulani kakusengenya wewe kadhaa na kadhaa." Au, "Fulani anakuchukia wala hakupendi." Kufitinisha huku kunaweza kuwa ni kwa kutamka maneno, au kwa kuandika au hata kwa kuonyesha ishara. Inaweza kuwa ni kufitinisha kwa kumsingizia mtu au hata kama huyo mtu alisema kweli  usemi huo haijuzi kufitinisha. Mtu kama huyu mwenye kufitinisha ni mwenye nyuso mbili anamkabili kila mmoja kwa uso mzuri kumbe hampendelei kheri, ni kama kinyonga anayebadilika rangi kwa hali anayojipendelea nafsi yake. Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuonya watu kama hawa kwa kusema: عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ :  ((‏ إِنْ شَرَّ النَّاسِ ذُو الْوَجْهَيْنِ الَّذِي يَأ...

'Uthmaan Bin 'Affaan (Radhiya Allaahu 'Anhu)

Jina Lake Na Ukoo Wake Jina lake ni ‘Uthmaan bin ‘Affaan bin Abul-‘Aas bin Umayyah bin ‘Abdus Shams, alikuwa Mquraysh wa Bani Umayyah. Ukoo wake na ule wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) unakutana kwa ‘Abdu Manaaf Alizaliwa katika mji wa Twaaif miaka sita baada ya mwaka wa Ndovu, sawa na 576 M Mama yake aliitwa Arwaa bint Kuraya bin Habiyb bin Abdus Shams, na bibi yake alikuwa Al-Baydha bint ‘Abdil-Muttwalib bin Haashim, shangazi wa Mjumbe wa Allaah. Ukoo Wake ‘Uthmaan alipewa lakabu ya Abu ‘Abdillaah (Baba ‘Abdullaah) na Abu ‘Amr. ‘Abdullaah alikuwa mtoto kwa Ruqayyah bintiye Mjumbe wa Allaah. ‘Abdullaah alifariki dunia alipokuwa na umri wa miaka sita yaani, mwaka wa nne wa Hijriyyah. Aidha ‘Uthmaan alipewa lakabu ya Dhun-Nurayn (mwenye nuru mbili) kwa sababu aliwaoa Ruqayyah na Umm Kulthuum mabinti wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Alikuwa mtu pekee aliyeoa mabinti wawili wa...