Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Kifo ni Mawidha

                              KIFO NI MAWAIDHA, MZAHA  MSIBANI  NI  UJINGA Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Naam anapofariki  mmoja wetu ni wajibu wetu kutafakari, leo ni mwenzetu kesho ni mimi au wewe, zidisha mema, acha mabaya ili ukutane na Mola wako ukiwa salama. Utani hauna nafasi msibani tena ni haramu na ujinga ulio pindukia, kwa nini usitafakari yale anayo kwenda kukutana nayo mwenzako huko kaburini nawe ukaanza maandalizi?. Amesema Allah mtukufu. الَّذي خَلَقَ المَوتَ وَالحَياةَ لِيَبلُوَكُم أَيُّكُم أَحسَنُ عَمَلًا ۚ وَهُوَ العَزيزُ الغَفورُ Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha (Almulqu Aya ya 2) Mazingatio ya waja wema walio tangulia (Salafi) juu ya kifo. قال عمر رضي الله عنه كفى بالموت واعظا. Amesema Umar Allah amridhie,...

Kujifuta Maji baada ya Kuoga na Kuchukua Wudhuu, Inajuzu?

Swali Je nikishaoga bila kujikausha maji, nikatawadha halafu ndio nikajifuta mwili kwa taulo safi , itakuwa nimetengua udhu wangu? Au ni lazima nioge, nijikaushe kwanza kabla ya kutawadha? Jibu  Hakika kila ‘Ibaadah katika Uislamu ina utaratibu na nidhamu yake. Na wudhuu pia una utaratibu wake na vitu ambavyo vinatengua wudhuu huo. Ikiwa hakuna kitu chochote cha kutengua wudhuu basi jambo  hilo litakuwa ni sawa. Tukija moja kwa moja katika swali lako ni kuwa unaweza kuoga, kisha ukatawadha na mwisho ukafuta maji na wudhuu wako utakuwa ni sahihi kabisa. Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake Al-Mughniy, anasema: “Hakuna tatizo kukausha viungo kwa kutumia taulo baada ya kuoga au baada ya Wudhuu” Haya ndio yaliyopokelewa kutoka kwa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah). Imepokewa pia kuwa ‘Uthmaan bin ‘Affaan, Hasan bin ‘Aliy, ‘Aliy bin Abi Twaalib, Anas na Maswahaba wengine kuwa walikuwa wakitumia taulo kujikausha baada ya wudhuu.” Shaykh Ibn ‘Uthaym...

Kutengukwa na Wudhuu katika Swalah ya Jamaa

Swali Je ikiwa  unaswali swalah ya  jamaa  na kati kati ya Swalah hiyo ukatengukwa na Wudhuu, Je  utahitajika kuondoka pale pale au usubiri umalize then utie udhu usali tena? ukizingatia jamii yetu wengi hatujui namna ya kupishana katika sala ukitokewa na udhuru. Jibu Swalah hili ni muhimu    na linahitaji kuonyeshwa kimatendo kwani huenda lisifahamike katika waraka.  Hivyo, itabidi katika Misikiti watu wafundishwe ili kusiwe na utata aina yoyote baada ya hapo. Kwani hili ni tatizo kubwa katika jamii zetu kujua namna ya kutoka pindi mtu anapotengukwa na wudhuu.  Lakini Insha’Allah tujaribu na tunamuomba Allah atupatie tawfiki katika  hilo . Pindi wudhuu unapovunjika inakuwa huwezi tena kuendelea na Swalah na inabidi uondoke ili ukachukue wudhuu na urudi uanze Swalah ile kuanzia mwanzo. Wudhuu unapomtenguka mmoja wetu inabidi akate Swalah na aanze harakati za kutoka ili aende kuchukua wudhuu mpya.  1.Hap...

Wudhuu unavunjika ikiwa Mtu hakujifunika Vizuri?

Swali Je unapotia udhu ukiwa umevaa Bukta au suruali kipande imekufika mapajani tu. Udhu unaingia Na vile vile  kama    uko tumbo wazi kitovu kinaonekana una hio suruali kipande tu. Udhu Unafaa? Jibu Kutokujifunika vizuri sio miongoni mwa vitu vinavyovunja wudhuu. Yafutayo ni mambo yanayovunja wudhuu na yasiyovunja. Yanayovunja wudhuu :   1-Kutokwa na mkojo, kinyesi    au hewa katika sehemu za siri kutokana na dalili katika Qur-aan:  ((أَوْ جَاء أَحَدٌ مَّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ)) ((au mmoja wenu ametoka chooni))  [Al-Maaidah:6] Vile vile Hadiyth:           ((لا يقبل الله صلاة أحدكم إذا أحدث   حتى يتوضأ   ))  البخاري   وسنن أبي داود     ((Allah Haikubali Swalah ya mmoja wenu akitokwa na haja hadi atawadhe))  [Al-Bukhaariy na Sunan Abu Daawuud] 2-Kutokwa na manii, madhii na ...

Mtu Mgonjwa afanye vipi Wudhuu na aswali vipi?

Swali Ndugu yetu mwanamume ni  mgonjwa (kilema)  yuko kwenye wheelchair, na mwenye kumuangalia hawezi kumuogesha kila siku, anamkogesha siku moja na siku ya pili anapumzika.    Maswali ni haya: 1)  Hawezi kila mara (au tabu  sana )  kumpeleka mswalani  na kumtilisha wudhuu. Je, afanye nini? Na hawezi kukaa na udhuu muda mrefu. Je, anaweza kuunga Sala? 2) Wakati mwingine huamka mgonjwa   akiwa  ameota  (Ndoto ya kutokwa manii) Je, lazima aoge josho?  na kama  hawezi afanye nini? Jibu Naam jambo la kwanza kabisa tu namuombea mgonjwa huyu kwa Allaah سبحانه وتعالى   Amuondoshee maradhi aliyonayo na ampe uzima na afya kamili kisha Amlinde na kila maradhi pamoja na wagonjwa wote wa Kiislamu. Jambo la Pili tunapenda kumpa bishara mgonjwa na jamaa zake kuwa huo ni katika mitihani ya Allaah  سبحانه وتعالى   ambao amekwisha andikiwa binaadam...