Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2017

Uchaji Mwema

KULINGANIA KWA ALLAAH (AD-DA’WATUL ILAA ALLAAH) Haja ya Watu katika Dini ni sawa na haja ya mwili kwa roho, kama ambavyo ikikosekana roho mwili unaharibika, hivyo hivyo Ummah utakapokosa Dini utaharibika. Rehma ya Allaah imeenea katika kila kitu, na rehma Zake kwa waja Amewatumia Mitume na Akawashushia vitabu ili wawafundishe watu wamjue Mola wao mwenye kuwaruzuku, wawabainishie Anayoridhia na wawalinganie katika kumtii na kumuabudu Yeye peke Yake bila ya kumshirikisha na chochote. Pia wawafahamishe Aliyowaandalia Mola katika Thawabu (ujira) kwa atakayemtii na adhabu kwa atakayemuasi. Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala): “Basi wako miongoni mwao ambao Allaah Amewaongoa na wako miongoni mwao ambao upotofu umethubutu juu yao.”   An-Nahl: 36 Kila walipodhoofika watu na kuingia katika shirki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Alituma Mitume wanaowalingania katika Tawhiyd na kumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) peke Yake. Walifuatana kuja Mitume na kila mmoja alitumwa kwa watu wa