Neema za Pepo Tuliyoahidiwa Maelezo ya Neema za Pepo tuliyoahidiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) yametajwa mno katika Qur-aan na Hadiyth, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala): إنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا . حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا. وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا. وَكَأْسًا دِهَاقًا. لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا جَزَاء مِّن رَّبِّكَ عَطَاء حِسَابًا. ((Hakika wenye taqwa [wamchao Allaah] wanastahiki kufuzu. Mabustani na mizabibu. Na wake waliolingana nao. Na bilauri zilizojaa. Hawatosikia humo upuuzi wala uongo. Malipo kutoka kwa Mola wako kipawa cha kutosha)) [An-Nabaa: 31-36] Anasema tena (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Suratul-Waaqiah وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ. أُوْلَئِكَ الْمُقَرَّبُونَ. فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ. ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ. وَقَلِيلٌ مِّنَ الْآخِرِينَ. عَلَى سُرُرٍ مَّوْضُونَةٍ. مُتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ
Anasema Allaah سبحانه وتعالى ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono yao , na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyokuwa wakiyachuma)) [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba". Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu". Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa, watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah سبحانه وتعالى Atawafunga midomo yao na kuviamrisha viungo vizungumze: عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى الله عليه وسلم، ف