Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2017

Je,Damu inazingatiwa ni Najisi?

 Je, Damu Inazingatiwa Kuwa Ni Katika Najisi? Damu ina vigawanyo:    1-  DAMU YA HEDHI :   Damu hii ni najisi kwa makubaliano ya Maulamaa. Dalili ya unajisi wake imekwisha elezewa nyuma.   2-  DAMU YA MWANADAMU [1]   Ni damu iliyosababisha mahitalifiano juu ya hukumu yake. Lililo mashuhuri kwa watu wa madhehebu ya kifiqhi ni kwamba damu ni najisi, lakini wao hawana hoja. Isipokuwa damu imeharamishwa kwa matini ya Qur-aan katika neno Lake Aliyetukuka:   ((قُل لاَّ أَجِدُ فِي مَا أُوْحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَى طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلاَّ أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ )) « Sema: Sioni katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayomwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu ». [2]   Kwa hiyo, wao wamewajibisha unajisi wake kutokana na kuharamishwa kwake, kamawalivyofanya katika pombe, na wala hayafichikani yaliyomo ndani yake. Lakini amenukuu zaidi ya

Baba yetu alitutupa sasa Amefariki ,tunataka kumsamehe tufanyaje?

SWALI   assalam alaykum warahmatuh-llah wabarakatuh. swala langu ni kuhusu babayangu, Aliyefariki kwanzia afariki sijawahi kumuombea mungu kwa sababu nilikuwa na uchungu sana wa kuwa hakuweza kutuangalia kwa lolote kwanzia kuzaliwa kwangu, na hata ndugu zangu.  Yaani ametutupa kwa kila kitu,kwahivyo hatukuwa na uhusiano hata kidogo twajua tu yule ndio baba yetu, kila nikikaa najiuliza kwa nini ametufanya hivi na alikuwa akijiweza hata kututazama alikuwa hakutaka tu!  Mpaka sasa ndio naona nimeanza kurudi nyuma manake nisingelipenda kumchukia mpaka ikafika hali ya zaidi ningelipenda kumuombea dua anisamehe na vile ashafariki mungu amsamehe. tafadha kwa kila shukrani munisaidie manake yananisumbua sana.ahsante.     JIBU Waleykum Salaam WarahmatulLaah Wabarakatuh   AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'an

Mawlid Kufanywa Wakati Msichana Anavunja Ungo Na Kusherehekea Jambo Hilo Na Mafunzo Kwa Biharusi

SWALI   Asalaam Aeikum Ndugu zangu katika Uislam Kwanza napenda kuchukua nafasi hii, kumshukuru Mwenyezi Mungu Subhaana waala Taala, kwa kunijaalia uzima na afya njema na uwezo wa kuweza kufahamu mtandao huu wa Alhidaaya. Katika siku ya leo napenda kuuliza maswali yafautayo ambayo yamekuwa yakinitatiza kichwani mwangu.   Kuna tabia katika baaaadhi ya jamii hapa kufanya sherehe, pengine husoma hata maulidi kwa mabinti zao baaada ya kuvunja ungo (kubalehe) Katika sherehe hizo pamoja na mambo mengine binti hufundishwa jinsi ya kuishi na mume pindi anapoolewa. Je mafunzo haya ni sahihi katika uislamu. Na kama si sahihi ni vipi binti wa kiislamu akikuwa hufunzwa   JIBU   AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.     Hakuna katika shariY’ah ya Kiislamu she

Nani vipenzi vya Allaah..?

Nani Vipenzi Vya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)? Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala): (( أَلا إِنَّ أَوْلِيَاء اللّهِ لاَ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ))  ((الَّذِينَ آمَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ)) لَهُمُ الْبُشْرَى فِي الْحَياةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ لاَ تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللّهِ ذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ))   (( Tanabahi!  Hakika vipenzi wa Allaah hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.   Ambao wameamini na wakawa wana taqwa.  Watapata bishara katika uhai wa dunia na ya Aakhirah. Hakuna mabadiliko katika Maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu adhimu. )) [Yuwnus: 62-64] Aayah hizi tukufu zinataja 'Vipenzi Vya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Ni nani basi hao vipenzi Vyake Mola Mtukufu? Je, ndugu Muislamu, unamiliki sifa za kuwa ni waliyyu-Allaah? (kipenzi cha Allaah)? Vipenzi vya Allaah ni kila aliyekuwa na sifa ya Aayah namba 63 nazo ni kuamini na kuwa na Taqwa, kwa maana kwamba wanafuata waliyoamrishwa na kujiepusha

Maonyo ya Allaah

Maonyo Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Kujiepusha Na Kughafilika Kwa Nafsi Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametuonya tusije kufikia hali ya nafsi kujuta kwa kutokana na kushughulika na mambo ya dunia ambayo ndio sababu kubwa ya kujikuta mtu yuko kwenye'ghaflah' (kughafilika na Aakhirah), kusahau kama mauti yako tayari kwa yule iliyomfikia ajali yake bila ya kujua lini au wapi ameandikiwa, kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala): (( وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ)) ((Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho. Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani. Hakika Allaah Ndiye Mwenye kujua, Mwenye khabari)). [Luqmaan: 34]. Kwa hiyo inapomfikia mtu ajali yake na roho inapotoka hapo nafsi tena hutambua kuwa yale yaliyokuwa yakimshughulisha duniani hayana tena faida naye wala hayawezi kumsaidia wakati huu, ndipo hubaki kujuta na kutambua kuwa yupo katika hasara kubwa!