Madhara Ya An-Namiymah (Kufitinisha ) - Vipi Kutibu An-Namiymah? Mafunzo yafuatayo yataweza Inshaa-Allaah kutibu maovu ya An-Namiymah ikiwa yatatekelezwa na inampasa kila mwenye tabia hii haraka ajifunze ili kujiepusha na maouvu haya yanayosababisha ufisadi na chuki baina ya ndugu Waislamu. Tutambue kuwa hii ni moja wapo ya jihadi ya nafsi kwa kujiepusha na maovu yanayoamrishwa na nafsi, ambayo ni jihadi bora kabisa na itamuweka Muislamu katika Ridhaa Ya Mola wake Mtukufu. Amesema Mtume (Swalla-Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kupitia usimulizi wa Fadhwaalah bin ‘Ubaydullaah (Radhiya Allaahu ‘anhu): (( ألا أخبركم بالمؤمن؟ من أمنه الناس علىأموالهم وأنفسهم، والمسلم من سلم الناس من لسانه ويده، والمجاهد من جاهد نفسه في طاعة الله، والمهاجر من هجر الخطايا والذنوب)) أحمد والحاكم , قال الألباني "إسناد صحيح" سلسلة الأحاديثالصحيحة ((Je, nikujulisheni kuhusu Muumini? Anayeaminiwa na watu juu ya mali zao na nafsi zao. Na Muislmu anayeweka amani kwa watu kwa ulimi wake na
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq