Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Shukurani zote Anastahiki Allaah, Mola wa ulimwengu wote. Rehma na amani zimshukie Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ahli zake na Masahaba wake. Enyi Waislamu muogopeni Allaah kwa kadri Anavyopaswa kuogopewa. Allaah Amesema, “Enyi mlioamini ! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha ; wala msife ila nanyi ni Waislamu.” (Aal 'Imraan 3:102) Ucha Mungu ni dalili ya Iymaan. Kwani kwa ucha Mungu ndipo mtu anaweza kudumu katika njia iliyonyooka (iliyo sawa) Jueni kuwa muongozo sahihi ni muongozo wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Ubaya wa mambo yote ni uzushi, na kila uzushi ni uovu, na kila ovu linampeleka mtu motoni. Enyi Waislamu! Allaah Amewaumba viume ili wamuabudu na wafungamane na Amri Zake na makatazo Yake. Allaah Anasema, "Nami Sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi." (Adh-Dhaariyaat 51:56) Allaah pia Anasema, "Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi Aliye
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq