*Swali* Asalam alaykum, shekh :mm nna mchumba angu lkn anakua mgumu kuja kuleta posa nymbani, jee? nimsomee dua gani ili aweze Kuja haraka maana ni cku nyingi tena naomba unisaidie unifahamishe ustadh. *Majibu* Wa Aleykum Sallaam WarahmatulLaah Wabarakatuh BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa Ba’ad. *Maana ya Uchumba Kisheria* ✅Uchumba katika Uislamu ni pale *mwanamme anayetaka kuoa au jamaa zake au mtu yeyote aliyemwakilisha anapokwenda kwa wazazi wa msichana/Bint/Mwanamke* kuposa/kupeleka Barua na kukubaliwa. *✅Huo ndio unaitwa uchumba* ➡Ama kinyume na hivyo unakuwa ni urafiki baina ya mvulana na msichana. *Na hili katika Uislamu limekatazwa kwani ni Haramu* ✅Na hili limekatazwa kishari’ah. ➡Na hapo katika Swali lako umesema kwamba una Mchumba wako Lakini anakuwa mgumu *kuleta posa nyumbani* ina maana kuwa Huyo mwanaume *Kisheria si Mchumba wako kwasababu bado hajapeleka barua ya Posa nyumbani kwenu*
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq