SWALI Sababu gani ya kisheria inayopelekea mwanamke kutoa mimba na asipate madhambi...? MAJIBU Kutoa mimba ikiwa ni kabla ya kupuliziwa roho au baada ya kupuliziwa roho kisheria ni haraam. Wakati unaokubalika kutoa mimba ni pale tu itakapokuwa kuna dharura za kisheria ndipo panaweza kukubalika tena kwa masharti yake. Dharura hizo, ni kama kumehakikishika kuwa kuna uwezekana wa mama kufariki kwa kuwa na kiumbe hicho, au kuendelea kwake kuwa na mimba hiyo kutamletea mauti. Na isitoshe kukubalika huko, bali kumetakiwa uthibitisho huo utolewe na daktari mwenye kuaminika kabisa. Na muhimu kwanza atafutwe daktari Muislamu mwenye kuaminika, ikishindikana, basi daktari yeyote ambaye ni muaminifu sana. Ama kuitoa mimba tu kwa sababu ya kutotaka mtoto, au kukhofia riziki yake, au malezi yake, au kuchelea gharama za maisha kama kumsomesha, kumvisha, au kumlisha n.k. hayo yote hayaruhusiwi kisheria kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema: “Wala msiwaue wana wenu kwa kuogopa umasikin
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq