Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2018

Hukmu ya Ghiyba ( kusengenya )

  Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Maana ya Ghiybah: Kilugha:    Kila kilichokuwa hakipo mbele yako. Na imeitwa Ghiybah kwa kutokuweko anayetajwa wakati anapotajwa na wengine.  Kishariy’ah : Kumsengenya mtu asiyekuwepo kwa mambo ambayo atachukia kuyasikia. Na maana yake ametujulisha Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipowauliza Maswahaba: ((   أتدرون ما الغيبة؟))  قالوا: الله ورسوله أعلم؛ قال:   (( ذكرك أخاك بما   يكره  ...)) ((Je mnajua maana ya  Ghiybah?)) Wakasema: Allaah na Rasuli Wake wanajua. Akasema: ((Kumsema ndugu yako anayoyachukia …..))   [Al-Bukhaariy] Imaam An-Nawawiy amesema kuhusu Ghiybah: "Kumsema mtu nyuma yake kwa yale anayoyachukia." Akaendelea kusema: "Kumsema mtu kwa anayoyachukia ikiwa yanayohusu mwili wake, au Dini yake, au dunia yake, au nafsi yake, au umbile lake au tabia yake, au mali yake, au wazazi wake, au mtoto wake, au mke wake, au mtumishi wake, au nguo yake, a