Kuachilia ndevu ni wajibu kwa wanaume kwa dalili zifuatazo: 1- Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kuziachilia. Amri hii ni ya lazima, kwani hakuna kiashirio chochote kinachoigeuza na kuipeleka katika usunnah. Na kati ya amri hizo ni neno lake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): خالفوا المشركين: وفروا اللحى، وأحفوا الشوارب ((Kuweni kinyume na washirikina; fugeni ndevu kwa wingi na punguzeni masharubu)) [Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy (5892) na Muslim (259)] Na neno lake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): جزوا الشوارب، وأرخوا اللحى، خالفوا المجوس ((Kateni masharubu na ziachilieni ndevu; nendeni kinyume na wanaoabudu moto)) [Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Muslim (260)] 2- Ni kwamba kuzinyoa ni sawa na kujifananisha na makafiri kama inavyoonekana katika Hadiyth mbili zilizotangulia. 3- Ni kwamba kuzinyoa ni sawa na kuubadilisha Uumbaji wa Mwenyezi Mungu na kumtii Shaytwaan
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq