Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Jambo la kwanza, kubwa, na la msingi katika kulingania watu kumtii Allaah, na kwa nini ‘Aqiydah iwe mwanzo. ‘Aqiydah ni lazima ije mwanzo kwa sababu, kinachozusha mgawanyiko na maangamizi katika ulimwengu wa Kiislamu ni kukosekana ‘Aqiydah iliyo sahihi. Kwa Nini ‘Aqiydah Liwe Ni Jambo La Mwanzo ? Hakika ‘Aqiydah lazima ije mwanzo kwa sababu ni msingi wa Da’wah ya Mitume wote kama Allaah Alivotuma ujumbe Wake kupitia kwa Mitume Wake. Kama Anavyosema Allaah kwa kupitia kwa ulimi wa kila Mtume Aliyemtuma kwa watu wake: “Enyi watu! Muabuduni Allaah, hamna mungu isipokuwa Yeye” (Surat Huud 11: 84) ‘Aqiydah lazima ije mwanzo kwa ajili ya kuepukana na kizuizi cha kubakia motoni (Jahannam) milele na kujiepusha na adhabu hiyo. Hamujasikia maneno ya Allaah Aliyetukuka: “Hakika Allaah hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Allaah basi hakika amezua dhambi kubwa” (Suratun
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq