Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2018

Msimamo wa Ibn ´Uthaymiyn juu ya kuhifadhi picha kwa ajili ya kumbukumbu

Swali:  Ni ipi hukumu ya kuvaa mavazi yaliyo na picha ima ya mnyama au mtu? Jibu:  Haijuzu kwa mtu kuvaa mavazi yaliyo na picha ya mnyama au mtu. Haijuzu vilevile kuvaa koti, kofia au kitu kingine kilicho na picha ya mtu au mnyama. Hayo ni kwa sababu imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Hakika Malaika hawaingii katika nyumba ilio na picha.” Kwa ajili hii hatuonelei kuwa inafaa kwa yeyote kuhifadhi picha kwa ajili ya kumbukumbu, kama wanavyosema. Yule ambaye yuko na picha kwa ajili ya kumbukumbu basi ni lazima kwake kuichana. Ni mamoja awe ameihifadhi juu kwenye ukuta, albamu au kitu kingine. Kuihifadhi kunapelekea kuwakosesha watu wengine wa nyumbani Malaika kuingia nyumbani mwao. Hadiyth hii tuliyoiashiria imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mhusika:  Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn Marejeo:  Majmuu´-ul-Fataawaa (02/166-167)

Picha Ya Mtoto Kwenye Simu

Swali:  Nina picha za watoto wangu kwenye simu ya mkononi. Je, inajuzu? Jibu:  Haijuzu kuhifadhi picha kwa ajili ya kumbukumbu au kitu kingine. Inajuzu kuhifadhi picha kwa ajili tu ya dharurah ya maisha yako. Kuhusiana na picha kwa ajili mtu anapenda, sanaa au kumbukumbu haijuzu. Ni wajibu kuziharibu. Usiache picha isipokuwa umeiharibu, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mhusika:  Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

Je, ni dharurah kupiga picha nikawatumia wazazi wangu?

Swali:  Mke wangu anaishi pamoja nami Saudi na anataka kuwatumia mzazi wake picha wanaoishi Misri ili apate utulivu. Na nimesikia Fatwa kuwa picha kwa ala ya picha ni Haramu. Je, hii ni dharurah? Jibu:  Hii sio dharurah. Haifai kwake kutuma picha yake, sawa kwa mama yake wala asiyekuwa mama yake. Kwani hii sio dharurah. Amuandikie [barua], aongee nae kwenye simu. Alhamduli Allaah. Ama kutuma picha haijuzu. Mhusika:  Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz Marejeo:  Nuur ´alaad-Darb

Picha kwa aina zake zote ni haramu

Swali:  Ni ipi hukumu ya kupiga picha kwa simu kama tunavyoona [msikiti wa] Haram? Jibu:  Haijuzu kupiga picha, si kwa simu, camera, kuchora na kunakili. Picha ni haramu kwa aina zake zote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa salam) amewalaani watengeneza picha na kueleza kuwa ndio watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah. Aina zote za picha ni haramu. Hili linahusiana na picha za viumbe wenye roho. Ni mamoja iwe katika Haram au kwengine. Ijapokuwa picha Haram ni khatari zaidi. Kwa sababu kufanya maasi Haram ni kubaya zaidi kuliko kufanya maasi nje ya Haram. Mhusika:  Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

Nasaha kwa wapenzi wa picha

Swali:  Una nasaha yoyote kuwapa wale ambao wamekithirisha kupiga picha kwenye msiktii mtakatifu wa Makkah na imekuwa ni kama vile ni sehemu ya utalii? Jibu:  Picha ni haramu sawa kwenye msikiti wa Makkah na kwenginepo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengeneza picha. Amesema kuwa wao ndio watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah. Wao ndio madhalimu wakubwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth ya kiungu ya kwamba Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema: “Ni nani dhalimu mkubwa ambaye anaumba kama viumbe Wake.” Bi maana watengeneza picha. Picha ni haramu. Imeharamishwa vibaya sana. Ni dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa. Zikipigwa kwenye msikiti mtakatifu wa Makkah khatari inaongezeka: إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ الَّذِي جَعَلْنَاهُ لِلنَّاسِ سَوَاءً الْعَاكِفُ فِيهِ وَالْبَادِ ۚ وَمَن يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍ بِظُلْمٍ نُّذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ “Hakika wale waliokufuru n

Filamu na Anaashiyd kwenye vituo vya majira ya joto

Filamu na Anaashiyd kwenye vituo vya majira ya joto Swali 2:  Kwenye majira ya joto kunachezwa filamu na Anaashiyd. Ni yapi maoni yako juu ya hilo? Jibu:  Ni wajibu kwa wasimamizi wa vituo vya majira ya joto kusitisha vitu vyote visivyokuwa na faida au vyenye madhara kwa wanafunzi. Wawafunze Qur-aan, Sunnah, Hadiyth, Fiqh na lugha ya kiarabu. Yanatosheleza na kwa kule kuchukua wakati. Wanatakiwa kuwafunza pia elimu ambayo itakuja kuwanufaisha katika dunia kama mfano wa kuandika, hesabu na ujuzi wenye faida. Mambo yanayoitwa “burudani” hayatakiwi kuwepo kwenye barnamiji [1] . Yanapoteza wakati. Pengine hata yakawasumbua na lile lengo lililowaleta. Miongoni mwa mambo hayo ni filamu na Anaashiyd. Haya si jengine isipokuwa ni pumbazo na mchezo. Ukiongezea juu ya hilo yanawafanya wanafunzi kuangalia michezo ya kuigiza na kusikiliza muziki unaorushwa kwenye vyombo vya khabari. [1]  Shaykh Swaalih al-Fawzaan amesema: “Kitu ambacho inatakikana kukisisitiza ni yale ambayo vijana wengi w

Kipi kinachoadhibiwa ndani ya kaburi?

Kipi kinachoadhibiwa ndani ya kaburi? Adhabu ya kaburi inakuwa kwenye kiwiliwili na roho vyote viwili, roho peke yake au kiwiliwili tu? Je, kiwiliwili kinashirikiana na roho katika kuhisi neema na adhabu kwenye kaburi? Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema baada ya kuulizwa swali hili yafuatayo: “Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wamekubaliana juu ya kwamba adhabu na neema inakuwa kwenye roho na kiwiliwili vyote viwili. Roho inaneemeshwa na kuadhibiwa peke yake na inaneemeshwa na kuadhibiwa pamoja na kiwiliwili. Kiwiliwili kinaweza kuhisi neema na adhabu pasi na roho? Ahl-us-Sunnah wal-Hadiyt na wanafalsafa wana maoni mawili yanayojulikana juu ya suala hili. Katika suala hili kuna maoni mengine vilevile yasiyokuwa na nguvu ambayo sio katika maoni ya Ahl-us-Sunnah wal-Hadiyth. Kuna wanaosema kuwa neema na adhabu inahusiana na roho peke yake pasi na kiwiliwili. Haya yanasemwa na wanafalsafa wanaokanusha kuwa viwiliwili vitafufuliwa. Hawa ni makafiri kwa maafikiano ya waislamu. Wanaf

al-Fawzaan akielezea rai tatu tofauti za Ahl-us-Sunnah kuhusu darsa na mawaidha ya video na kwenye TV

Swali:  Inajuzu kurekodi kanda za mihadhara kwa njia ya video na kuuza kanda hizi katika baadhi ya maduka ya rekodi? Pamoja na kuzingatia ya kwamba kunakuwepo vilvile kanda za maonyesho na tamthiliya/filamu zinazoitwa “tamthiliya/filamu za Kiislamu”. Ni yepi maoni yako juu ya hilo? Jibu:  Masuala ya kurekodi mihadhara kwa njia ya video au kwa njia ya TV ni jambo ni jambo limefanyiwa utafiti. Upande mmoja ndani yake kuna manufaa; kuwafikishia watu kheri na kuwafundisha. Lakini upande mwingine kuna madhara vilevile; picha. Kwa hivyo masuala haya ni yenye mashaka. Iwapo tutatazama zile kheri zinazopatikana ndani yake tunaweza kusema kwamba kheri inatakiwa kuenezwa. Lakini tukitazama picha zinazopatikana ndani yake tunaweza kusema kuwa haya ni madhara na wala haijuzu kuchukulia wepesi suala la picha ambalo limeharamishwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hiyo jambo hili mimi nimenyamaza. Kutokana na ninavyojua wanachuoni wana maoni tatu: 1- Wapo ambao wanaonelea kuwa ni ha

Kurecord kwa Video inafaa?

Swali:  Ni ipi hukumu ya kuchukua mihadhara na semina kwa kutumia kifaa cha video camera? Jibu:  Naona kuwa hakuna ubaya kurekodi mihadhara na semina kwa kifaa cha video camera haja ikipelekea kufanya hivo au manufaa yakapelekea kufanya hivo kutokana na yafuatayo: La kwanza: Kurekodi ambako ni moja kwa moja (live) hakuingii katika kuiga uumbaji wa Allaah. Hilo liko wazi kwa wale wenye kuzingatia. La pili: Picha haionekani kwenye mkanda. Kwa hivyo hakuna kitendo cha kuhifadhi picha. La tatu: Tofauti iliyopo ya kuingia video camera katika kuiga uumbaji wa Allaah – hata kama hilo linarithisha kufanana – hakika haja au manufaa yaliyohakikiwa hayafanyi tofauti kuisha katika jambo ambalo haijabaini namna ya kukatazwa kwake. Rejea Majmuu´-ul-Fataawaa (02/284) Mfasiri Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn

Swalah ya Eid

Hukumu ya swalah ya ´Iyd Ndugu muislamu! Jifunze baadhi ya hukumu muhimu unazotakiwa kuzijua zinazohusiana na mwezi huu mtukufu. Swalah ya ´Iyd Kwa mujibu wa wanachuoni wengi swalah ya ´Iyd ni faradhi kwa baadhi ya waislamu. Inajuzu kwa baadhi kutoiswali. Hata hivyo imependekezwa kuihudhuria na mtu kushirikiana na ndugu zake waislamu. Ni Sunnah iliyokokotezwa isiyotakikana kuachwa isipokuwa kwa kuwepo udhuru wa Kishari´ah. Baadhi ya wanachuoni wanaonelea kuwa ni lazima kwa waislamu wote kuiswali kama swalah ya Ijumaa. Wanaume wote katika mji na ambao wana majukumu juu ya matendo yao ni lazima waiswali. Maoni haya ndio yanaonekana kuwa dalili yenye nguvu na ilio karibu zaidi na usawa. Ni Sunnah kwa wanawake kuihudhuria. Lakini wanatakiwa kuzingatia kujisitiri vizuri na kutojitia manukato. Imethibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim ya kwamba Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametuamrisha kuwatoa nje siku ya ´Iyd mbili wan

Kutengukwa Na Wudhuu Katika Swalah Ya Jamaa

SWALI Kama unasali jamaa kati kati ukatengukwa na udhu utahitajika kuondoka pale pale au usubiri umalize then utie udhu usali tena? ukizingatia jamii yetu wengi hatujui namna ya kupishana katika sala ukitokewa na udhuru.   JIBU     Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.   Swalah hili ni muhimu    na linahitaji kuonyeshwa kimatendo kwani huenda lisifahamike katika waraka. Hivyo, itabidi katika Misikiti watu wafundishwe ili kusiwe na utata aina yoyote baada ya hapo. Kwani hili ni tatizo kubwa katika jamii zetu kujua namna ya kutoka pindi mtu anapotengukwa na wudhuu. Lakini Insha’Allah tujaribu na tunamuomba Allah atupatie tawfiki katika  hilo. Pindi wudhuu unapovunjika inakuwa huwezi tena kuendelea na Swalah na inabidi uondoke ili ukachukue wudhuu na urudi ua

Kuichelewesha Zakaatul-Fitwr

SWALI: Nilikuwa katika safari na nikasahau kutoa Zakaatul-Fitwr. Nikuwa nasafiri usiku wa 27 Ramadhwaan na hatukutoa Zakaatul-Fitwr hadi leo. JIBU: Ikiwa mtu amechelewesha Zakaatul-Fitwr japokuwa alikumbukua kuitoa, basi atakuwa ni mtenda dhambi na itampasa atubie kwa Allaah na kuilipa kwa sababu ni kitendo cha ibada ambacho kinabakia kuwajibika japokuwa muda wa kutoa umepita kama mfano wa Swalaah. Lakini kama muulizaji huyu alivyotaja kuwa alisahau kuilipa kwa wakati wake, hivyo hakuna dhambi juu yake lakini lazima ailipe. Kusema kuwa hakuna dhambi juu yake ni maana kwa ujumla kutokana na dalili inayoonyesha kuwa hakuna dhambi kwa mtu anayesahau lakini bado atakuwa amewajibika kuilipa kutokana na sababu zilizotolewa juu. Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.   [Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah  (2867)]

Inafaa Mtoto Wa Kike Kumlipa Baba Yake Zakaatul-Fitwr?

SWALI:   Mtoto wa kike anaweza kumlipia baba yake Zakaatul-Fitwr?   JIBU:   Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu- Allaah) amesema:   Yeyote anayelipa Zakaatul-Fitwr kwa mtu na ambaye hakuwajibika kumlipia lazima achukue ruhusa yake. Hivyo ikiwa Zayd anamlipia 'Amr bila ya ruhusa yake, itakuwa ni batili, kwa sababu Zayd hakuwajibika kumlipia 'Amr Zakaatul-Fitwr.   Ni muhimu kwamba niyyah sahihi itiwe ikiwa kwa ajili ya kujitolea mtu binafsi au kumlipia mtu mwignine. Hii ni kutokana na hukmu inayojulikana sana kwa Fuqahaa ambao wameiita 'taswarruf al-fudhwuwl' ikimaanishwa suala wakati mtu anamfanyia mwenziwe kitendo bila ya ruhusa yake, je huwa kitendo kinasihi kikamilifu au inategemea ruhusa na ridhaa ya mtu mwengine?    Kuna ikhtilaaf baina ya ‘Ulamaa katika mas-ala haya. Na rai iliyo sahihi kabisa ni kwamba inasihi ikiwa mtu mwengine ametoa ruhusa. Na Shaykh amenukuu Hadiyth ya Abu Hurayrah alipozungumza na Shaytwaan alipokuwa akiilinda Zakaah.   Hii inat

Zakaatul-Fitwr Kwa Ajili Ya Mtoto Aliye Tumboni

SWALI: Zakaatul-Fitwr ilipwe kwa ajili ya mtoto aliye bado tumboni mwa mama?   JIBU: Inapendekezeka kulipa kwa sababu 'Uthmaan (Radhiya Allaahu 'anhu) alifanya. Lakini sio fardhi bali ni jambo linalopendezeka tu. Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam. [Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah]

Kutoa Kiwango Cha Zakaatul-Fitwr Katika Vyama Vya Misaada Mwanzo Wa Ramadhwaan

SWALI:   Vyama vya misaada vinaruhusiwa kupokea Zakaatul-Fitwr mwanzo wa Ramadhwaan ili waweze kuigawa kwa mpangilio mzuri kabisa?   JIBU:   Sifa Zote Ni Za Allaah   Ikiwa hakuna watu masikini katika eneo au wale watakaopokea hawaihitajii hasa, na hawatoila bali wataiuza kwa nusu ya thamani yake, na ikiwa ni tabu kupata maskini na wanaohitaji watakaoila, hivyo inaruhusiwa kuituma nje ya nchi. Inaruhusiwa kutoa thamani (ya Zakaatul-Fitwr) mwanzo wa mwezi kwa dalali ambaye atainunua (Zakaatul-Fitwr) na kuituma kwa watu wanaostahiki wakati huo unapotakiwa kulipwa, ambao ni usiku kabla ya 'Iyd au siku mbili kabla yake.   Na Allaah Anajua zaidi   [Al-Fataawa Al-Jibriyn fil A'maal Ad-Da'wiyyah li Fadhwiylat Ash-Shaykh 'Abdillaah bin Jibriyn Uk. 33]  

Hukmu Ya Asiyelipa Zakaatul-Fitwr Japokuwa Ana Uwezo

SWALI: Nini hukmu ya mwenye uwezo wa kutoa Zakaatul-Fitwr lakini hatoi? JIBU: AlhamduliLLaah,   Asiyetoa Zakaatul-Fitwr lazima afanye Tawbah kwa Allaah na aombe maghfirah kwa sababu anapata dhambi kuizuia. Itambidi pia ailipe kwa wanaostahiki kuipokea, lakini ikiwa baada ya Swalaah ya 'Iyd itahesabika kama ni sadaka ya kawaida. Wa biLLaahi at-tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam .   [Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah]

Zakaatul-Fitwr Ni Fardhi Kwa Masikini Pamoja Na Familia Yake?

SWALI: Mtu masikini mwenye majukumu ya familia yake ambayo ni miongoni mwa mama, baba na watoto. 'Iydul-Fitwr inawadia naye ana swaa’ (pishi moja)  tu ya chakula. Amlipie nani?  JIBU: AlhamduliLLaah Ikiwa hali ya masikini huyu ni kama ilivyoelezewa katika Swali, hivyo alipe swaa’ (pishi – kilo 1 ½ - 3) ya chakula kwa ajili yake kwani ni ziada ya mahitajio yake na mahitajio ya wale ambao ni wajibu wake kuwahudumia mchana na usiku wa 'Iyd, kwa sababu  Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Anza kwa nafsi yako kisha kwa wanaokutegemea))  [Al-Bukhaariy 2/117, 6/190, Muslim 2.717, 718, 721, 1034, 1036, 1042]   Kuhusu wanaomtegemea ikiwa hawana chochote cha kujitolea katika Zakaah kwa nafsi zao wenyewe, basi hawakuwajibika kulipa kwa sababu Allaah Anasema:  ((Allaah Haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo)) [2: 286]   Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna sadaka isipokuwa kwa yule mwenye uwezo)) [

Kutoa Zakaatul-Fitwr Kwa Kiwango Zaidi Ya Anachostahiki Maskini Na Kutoa Siku Kumi Kabla Ya Ramadhwaan Kumalizika

SWALI: Assalam alaykum, naomba kuuliza, 1. _*ikiwa mie natakiwa kutoa Zakaatul fitr yenye thamani ya pesa zaidi ya laki moja na nayelenga kumpa ana hitajio la juu sana, yajuzu kumpatia zaka iyo siku 10 kabla ya Eid el fitr?*_   2. _*je naweza kumpatia kiasi cha zaidi ya ile ninayowajibikiwa kutoa nikiwa na niya ya kumfanya awapendezeshe watu wa nyumbani kwake na awalishe pia?*_   JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa   aalihi   wa   sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.   Wa 'Alaykumus Salaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh,   Zakaatul-Fitwr hutolewa chakula na si pesa kwa mujibu wa Ahaadiyth zilizopokelewa katika mlango huo.   Dalili:   Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma) amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliifanya kutoa swaa' (pishi) ya tende au swaa

Ndoa ya Waliozini kwa mtazamo wa Ahlu Sunnah

BismiLlaahi Ar-Rahmaanir Rahiym   Tunachukuwa fursa hii kuweka wazi madhehebu ya Ahlus Sunnah katika maudhui ya kujuzu au kutokujuzu kuoana waliozini.   Sababu iliyopelekea kuandika makala hii ni baada ya kusingiziwa wanavyuoni wa Ahlus Sunnah kuwa wana msimamo sambamba na msimamo wa kiibadhi ambao ni kutojuzu ndoa ya waliozini.   Singizio hili limetolewa na mmoja wa waandishi wa kiibadhi wa makala mbali mbali, kwa kusema “ riwaya tulizozinukuu humu zote zinatoka katika vitabu vya kisuni, kwa sababu wengine hudhani labda ni msimamo wa Ibadhi tu . ”   Haya ni maneno yanayoashiria wazi kuwa Ahlus Sunnah nao huharamisha moja kwa moja kama wanavyoharamisha maibadhi kuoana wale waliofanya zinaa na hili linatokana na suala la muulizaji kama lilivyotangulia.   Na ifahamike kuwa lengo langu si kuelezea dalili za Ahlus Sunnah katika suala hili kwani makala itarefuka mno, na lengo khassa ni kueleza uhakika wa suala hili katika madhehebu ya Ahlus Sunnah ambayo yanajumuisha madhehebu

Usiku wa Qadar

Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Usiku wa Qadar Usiku wa Qadar ndio usiku bora kabisa. Ndani yake Allaah ameteremsha Qur-aan. Ameeleza (Subhaanah) ya kwamba ni usiku ulio bora kuliko miezi elfu moja na umebarikiwa na kwamba ndani yake kunabainishwa kila jambo la hekima. Allaah (Subhaanah) amesema mwanzoni mwa Suurah “ad-Dukhaan”: حم وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ أَمْرًا مِّنْ عِندِنَا ۚ إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ “Haa Miym. Napaa kwa Kitabu kinachobainisha! Hakika Sisi tumeiteremsha katika usiku uliobarikiwa – hakika Sisi tumekuwa [daima ni] wenye kuonya [watu] – Humo [katika usiku huo] hupambanuliwa kila jambo la hikmah na jambo [Tunalokadiria ni lenye] kutoka Kwetu – hakika Sisi [daima] ndio wenye kutuma [wajumbe Wetu kwa mafunzo na mwongozo]. – Ni Rahmah kutoka kwa Mola wako, hakika Yeye ni Mwenye kusikia y

Katika Dini Mtazame Aliye Juu Yako – Katika Dunia Mtazame Aliye Chini Yako

Allaah (Ta´ala) amesema: وَلَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّنْهُمْ زَهْرَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا لِنَفْتِنَهُمْ فِيهِ ۚ وَرِزْقُ رَبِّكَ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ  “Na wala usikodolee macho yako kwa yale Tuliyowastareheshea baadhi ya watu miongoni mwao, kwani hayo ni mapambo ya uhai wa dunia tu ili Tuwafitinishe kwavyo. Na riziki ya Mola wako ni bora zaidi na ni yenye kubakia.” (20:131) Usiikodolee macho dunia, ukataka kuwapokonya wenye nayo na ukatamani kupata mfano wa walionayo. Kuhusu dunia mtazame yule aliye chini yako. Kuhusu Dini mtazame yule aliye juu yako ili uweze kushindana naye. Dunia mtazame yule aliye chini yako ili upate kuona neema za Allaah juu yako. Kuna watu wako chini katika maisha haya ya dunia, sawa inapokuja katika mali, siha, afya na nyumba. Utapowatazama watu hawa [na ukaona tofauti kubwa kati yako wewe na wao], basi zikumbuke neema za Allaah juu yako na uziadhimishe na kuzishukuru. Marejeo:  adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid

Fadhila za Kutoa

Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh 125- Asmaa´ bint Abiy Bakr (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kunambia: “Toa au chinja. Usihesabu Allaah akaanza kuhesabu Anavyokupa na usizuie Allaah akaanza kuzuia kutoka kwako.” [1] 126- Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: “Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupatapo kuombwa kitu kamwe akasema: “Hapana”. [2] 127- Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Ambaye yuko na kipando cha ziada basi ampe ambaye hana kipando na ambaye yuko na chakula cha ziada ampe ambaye hana chakula.” Alifanya tukaona kuwa hakuna yeyote katika sisi ambaye yuko na haki zaidi ya kile chenye kutosheleza.” [3] 128- Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: “Kuna mbedui alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuomba kitu ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamrisha apewe kondoo 40.000. Mtu y