Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2019

Fadhila za Kusuluhisha Waliogombana

Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa  aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad. Naam, Ndugu zangu katika Imaani Muda huu napenda kuchukua Fursa hii kufikisha kwenu japo kwa Uchache Darsa letu lenye anuani isemeyo Fadhila za Kusuluhisha Waliogombana ➡Anasema Allaah سبحانه وتعالى Kwamba⤵ ((لاَّ خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلاَّ مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلاَحٍ بَيْنَ النَّاسِ وَمَن يَفْعَلْ ذَلِكَ ابْتَغَاء مَرْضَاتِ اللّهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمً )) ((Hakuna kheri katika mengi ya wanayoshauriana kwa siri, isipokuwa kwa yule anayeamrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Allaah basi Tutakuja mpa ujira mkubwa)) ↪Suratul An-Nisaa Aya ya 114. ➡Na kasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwamba⤵ ((ألا أخبركم بأفضل من درجة الصيام والصلاة والصدقة ؟ إصلاح ذات البين وفساد ذات البين هي الحالقة))  رواه

Hukmu ya Wanaume kupiga Makofi katika Mihadhala

Swali Nini hukumu ya kupiga makofi wanaume wanapokuwa wanapongeza mtu au kushangilia jambo kama tunavoona ktk mihadhara, makongomano, semina, mijadala na midahalo ya dini? Hili limekuwa jambo la kawaida hata ktk TV za Kiislamu tunazoona.     Jibu Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:   وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِندَ الْبَيْتِ إِلَّا مُكَاءً وَتَصْدِيَةً     (( Na haikuwa Swalaah [ ‘ibaadah ] zao [ makafiri ] kwenye Nyumba [ Tukufu yaani Ka’bah ] isipokuwa ni miruzi [ mbinja ] na kupiga makofi )).  [Al-Anfaal: 8: 35].     قال الرسول صلى الله عليه وسلم: (مَنْ نَابَهُ شَيْءٌ فِي صَلَاتِهِ   فَلْيُسَبِّحْ فَإِنَّهُ إِذَا سَبَّحَ الْتُفِتَ ،، و إِنَّمَا التَّصْفِيقُ   لِلنِّسَاءِ ).  رواه البخاري (684) ومسلم (421)   “Mtume ( Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam ) amesema : (( Atakayetanabahi kitu katika Swalah yake , alete tasbiyh [ Aseme Subhaana-Allaah ] kwani anapoitamka , humvutia mtu atanabahi , na hakika kupiga makofi ni kwa ajil

Anaishi na Mwanaume Mkristo Je akifunga Ramadhaan Swawm itaswihi?

Swali Swali langu ndugu zangu  katka iman  ..inakuaje binti waislam anaishina mkristu na amezaa nae watt zaidi ya mmoja alafu anajiweka katk kuufunga mwezi waradhani nabado anaendelea kuishi nae na anahudumiwa kama mke Je hukumu yake nini au je inaswihi au laa Jibu Naam Swawm yake inaswihi Naam kwanza kabisa ni WAJIBU  kwa Muislam kufunga Mwezi wa Ramadhaan. Maulamaa wamekubaliana kufunga ni wajibu kwa Muislam mwenye akili timamu, Baleghe, mwenye afya na mkazi wa mji. Tukiongezea wanawake waliotwaharika na hedhi na nifasi. Kwahiyo ikiwa wewe Mwanamke ni Muislam basi ni Lazima Ufunge Mwezi wa Ramadhaan na haijalishi unaishi na kafiri. Jambo lingine ni kwamba ni HARAMU kwa Mwanamke wa Kiislamu kuishi na Mwanaume Mkristo kama Mumewe. Hapo Mwanamke unakuwa unafanya Zinaa na Allaah amekataza Zinaa na ni Uchafu. Allaah(Subhaana wa Taala) Ametoa ruhusa kwa mwanamume wa Kiislamu tu kumuoa mwanamke wa Kitabu (Mkristo au Myahudi). Hata hivyo Allaah (Subhaana wa Taala) hakuliacha jambo

Mambo yanayofaa Kufanywa na Mwenye Kufunga

                                           Mambo yanayofaa Kufanywa na Mwenye Kufunga 1. Anaruhusiwa kujisuuza kichwa na maji ya baridi. 2. Kusukutua na maji bila kuyamiza na kutiya maji puani bila kuingiya ndani ya mwili. 3. Kuumikwa ama kutoa damu kwa ajili ya matibabu. 4. Kumbusu au kumgusa mke wako bila matamanio kwa mwenye kuweza kujizuwiya. 5. Mwenye kuamka asubuhi na akiwa katika janaba. 6. Kuchelewesha kufungua swawm mpaka saa ya kula daku. 7. Kutumia mswaki, manukato, wanja, dawa ya macho na kudungwa sindano kwa ajili ya matibabu. Na  Allaah  anajua  zaidi

Mambo Sita Yanayobatilisha Swawm

Mambo Sita Yanayobatilisha Swawm                                                                                                           1. na 2. Kula au kunywa kwa kukusudia. 3. Kujitapisha kusudi. 4. na 5. Mwanamke atakapopata ada yake mwezi akiwa katika swawm. 6. Kitendo cha Jimai. Mambo Yaliyopendekezwa kwa Mwenye Kufunga Imependekezwa kwa mwenye kufunga afuate Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) katika kujitayarisha na swawm yake nayo ni haya yafuatayo; 1. Kula daku Amehadithia Anas (Radhiya Allaahu ´anhu) Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) amesema: ‘’Kuleni daku, kwani kula huko daku kuna baraka.”  [Imeripotiwa na Imaam Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Nasaa’y na Ibn Maajah]. Na ‘’kuleni daku’’ hata kama kwa kunywa maji inatosheleza. ´Abdullaah Ibn ´Amr amehadithia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema: ’’Kuleni daku japo kwa kunwa tama la maji.’’  [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swa

Mambo yenye Umuhimu kwa Ujumla wa Kutekeleza ´Ibaadah ya Swawm (Kufunga)

              Mambo yenye Umuhimu kwa Ujumla wa Kutekeleza ´Ibaadah ya Swawm (Kufunga) 1. Niyyah. Allaah (Subhanahu wa Ta’ala) Amesema: وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاء وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ وَذَلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ “Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Allaah kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Swalah, na watoe Zakaah. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.”  (Suuratul Bayyinah 98 : 05) Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema: ’’Kila kitendo hulipwa (kutokana na) niyyah na kila mtu ni lili alilonuwiya.’’ Na niyyah mahala pake ni moyoni. Niyyah ya kufunga ni lazima iwe moyoni kila usiku kabla ya wakati wa Fajr kuingiya. Hafsah (Radhiya Allaahu ´anha) amesema mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema: ‘’Hana swawm asiyenuwia kufunga kabla ya fajr.’’  [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh al-Jamiy´ as-Saghiyr, na.6238. Pia imerikodiwa na Abu Dawuud, At-Ti

Mwanamke Mja Mzito (Mwenye Mimba) au Mwenye Kunyonyesha

                              Mwanamke Mja Mzito (Mwenye Mimba) au Mwenye Kunyonyesha Mwanamke mwenye mimba au mwenye kunyonyesha ambaye hana uwezo wa kufunga ama ambaye anahofia afya ya mtoto wake  anaweza asifunge, atalisha maskini mmoja na hawajibiki kuilipa siku aliyokula. Ibn ´Abbaas amesema: “Ruhusa amepewa mtu mzima mume au mke ambapo wataoneleya tabu kufunga, hawatofunga ambapo hawatopendeleya kufunga na watalisha maskini mmoja kwa kila siku ya kufunga. Kisha hawatalipa siku walizokosa kufunga hii iliondolewa baada ya Aayah hii: وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ “Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. (kwa kila siku).”  (Suuratul Baqarah 02 : 184) Baada ya hapo ikahakikishwa  kuwa mtu mzima mume au mke ambao hawawezi kufunga  na mwanamke mwenye mimba au mwenye kunyonyesha, ikiwa watahofia, hawatafunga na watalisha maskini kwa kila siku ambayo hawakufunga. [Msururu wa Riwaayah hii ni madhubuti imeripotiwa na Al-Bayha

Yanayomlazimu Mtu Mzima na Mwenye Ugonjwa wa kuendelea

                             Yanayomlazimu Mtu Mzima na Mwenye Ugonjwa wa kuendelea Asioweza kufunga, kwa ajili ya utu uzima au kwa ajili sababu nyenginezo, hatofunga badili yake atalisha maskini mmoja kwa kila siku aliokosa kufunga. Allaah (Subhanahu wa Ta’ala) Amesema: وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ “Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. (kwa kila siku).”  (Suuratul Baqarah 02 : 184) ‘Atwaa’ amesema alimsikiya Ibn ´Abbaas akisoma Aayah hii kisha akasema ‘’Haikuondolewa. Inawahusu watu wazima waume kwa wake ambao hawawezi kufunga. Ndio watalisha masikini mmoja kwa kila siku ambayo hawakufunga.”  [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl na.912 na Imerikodiwa na Imaam Al-Bukhaariy]. Na  Allaah  anajua  zaidi

Nani Anawajibika Kufunga?

                                                 Je,Ni nani Anawajibika Kufunga...? Maulamaa wamekubaliana kufunga ni wajibu kwa mwenye akili timamu, Baleghe, mwenye afya na mkazi wa mji. Tukiongezea wanawake waliotwaharika na hedhi na nifasi. Kwa wale ambao Swawm si wajibu juu yao ni wale ambao hawana akili timamu, hawajabaleghe. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema: “Kalamu (kurekodiwa ‘amali) imeinuliwa (hairekodi) kwa watu watatu: anayepatwa na usingizi mpaka aamke, mtoto mpaka afike umri wa kubaleghe, na aliorukwa na akili mpaka atakapopata akili timamu.”  [Hadiyth imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jami´, na. 3513 na Imerikodiwa na Abu Daawuwd]. Ama kwa wale wasioweza kufunga  ni kutokamana na maneno Yake Allaah: فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ “Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini (akafunga baadhi ya siku); basi (akamil