Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2019

Madhambi Makubwa na Madogo

                                            MADHAMBI  MAKUBWA  NA  MADOGO Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Madhambi Makubwa Madhambi makubwa ni yale ambayo yametajwa katika Qur-aan na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam ) nayo ni yale ambayo mja anapoyafanya huwa na hukmu zifuatazo: 1-Madhambi ambayo Allaah Anaalaani kitendo chake. 2-Madhambi ambayo yamewekewa adhabu kali kama mfano mwenye kuzini na hali ameoa au ameolewa kupigwa mawe hadi kufa au kupigwa bakora 100 kwa asiyeoa au asiyeolewa. 3-Madhambi ambayo Anaghadhibika nayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala). 4-Madhambi ambayo Allaah Anamnyima Rahmah Yake mwenye kuyatenda. Hadiyth ifuatayo imeyaelezea baadhi ya madhambi hayo makubwa ambayo yanajulikana   Sab'ul-Muwbiqaat  (saba yenye kuangamiza). عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  عن النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ)) قَا

Maana ya Aya ya 103 katika Surat Al-An’aam yanayosema “Macho Hayamzunguki”

Maana ya Aya ya 103 katika Surat Al-An’aam yanayosema  “Macho Hayamzunguki” Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) amesema: “Na maana “Bila kuzunguka wala  kayfiyah  (kuzunguka vipi”, wao hawamzunguki Allaah (‘Azza wa Jalla), na kwamba wao wanamuona (Allaah) Subhaanahu bila ya kumzunguka. Na Allaah Mtukufu haiwezekani Yeye  kuzungukwa. Anasema Subhaanahu: وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا ﴿١١٠﴾ na wala hawawezi kufikia kuelewa chochote cha ujuzi Wake . [Twaahaa: 110] Na Anasema Jalla Wa ‘Alaa: لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ    Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote.  [Al-An’aam: 103] “Macho hayamzunguki” Maana yake (katika Aayah hiyo) ni kuwa, “Hayamzunguki Yeye (macho ya mtu)”, na wala maana yake si “Hayamuoni.” Kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa) Hakusema, “Hayamuoni Yeye macho.” bali Kasema,  “Macho hayamzunguki.”  Kudiriki ni kitu na kuona ni kitu kingine. Hayo (macho) yanamuona Subhaanahu bila kumzung

Tahiyyatul-Masjid inaweza kuswaliwa katika Nyakati zilizokatazwa?

Swali Kuna mazungumzo mengi kuhusiana na Tahiyyatul Masjid. Kuna wanaosema haipaswi kutekelezwa nyakati zilizokatazwa kuswaliwa Swalaah, kama zile nyakati za kuchomoza jua, na kuzama jua. Wengine husema inaruhusiwa maadam sababu ya kuswaliwa Swalaah hiyo, haijawekewa vikwazo vya nyakati zozote, na inapaswa kuswaliwa hata kama nusu ya jua litakuwa limeshazama. Naomba ufafanuzi wa kina kwa suala hili. Jibu Naam kuna Ikhtilaaf  baina ya Wanachuoni kuhusu jambo hili. Lakini mtazamo sahihi (Kauli yenye nguvu) ni kuwa, Tahiyyatul-Masjid ni rukhsa kuswaliwa katika nyakati zote, hata kama ni baada ya Al-Fajr au hata baada ya Al-‘Aswr kutegemea maana ya maneno ya jumla ya Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)⤵ “Atakapoingia yeyote katika nyinyi Msikitini, hapaswi kukaa hadi aswali rakaa mbili.” ↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim Vilevile, hiyo ni Swalaah ambayo ina sababu ya kuitekeleza kama vile Swalaah ya kutufu ‘Swalaatut-Twawaaf’ (Rakaa mbi

Mke amefariki hali ya kuwa hajamaliza mahari, Je mke atakaa eda na kukamilisha Mahari?

*Swali* Mume ameoa siku ya Ijumaa, na akadhamiria kumfuata mkewe siku ya jumapili, ila kwa Qadar ya Allaah yule Mume akafariki Siku ya Jumamos na hali ya kua hajamaliza Mahari, na wala hajamuingilia mkewe. 1.Je,mke huyo ipo haja amaliziwe mahari yake  au yeye mke ndio arejeshe Mahari? 2.Je mke atakaa Eda?  Na ni Eda gani? 3.Je,mke huyo atarithi kwa Mumewe aliyefariki?  *Majibu* Bismillaahir Rahmaniir Rahiim Kwanza kabisa shukrani kwa Swali lako, ila kwanza kabla sijakujibu swali lako naomba mjihadhali sana na Maswali ya kutunga. Mke atakamilishiwa mahari yake kamili. Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliulizwa kuhusu mwanamme ambaye alimuoa mwanamke na hakutaja mahari yake au kumuingilia kabla ya kufa (mwanamme). Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) akajibu: "Anapaswa kupewa mahari yake kama wanawake mfano wake; si ziada wala pungufu, na vilevile anapaswa kukaa eda, na ana haki ya Miyraath. Ma'quwl bin Sinaan Al-Ashja'iy (Radhwiya Allaahu '

Je, Wanandoa waliosilimu watafunga ndoa upya?

*Swali* Swali, kwaupande wa wenzetu wakristo Kwa imani yao wao walikuwa wanaishi pamoja wakiwa wamefunga Ndoa kanisani ila Baada ya Miaka miwili Wakapata Dawa ikawaingia wakaamua kuslimu na kuwa Waislam Je inabidi Wafunge Ndoa Upya Au wanaendelea na Ndoa ile ile walio funga Kanisan? *Jibu* ✅Ama kuhusu swali hili ni kuwa mtu aliyesilimu na mkewe, Uislamu unaikubali ndoa yao waliyofunga kanisani au kimila ikiwa ndio inayotambuliwa kiada wakati huo walipooana. ➡Hivyo, wanandoa hao hawana haja kufunga ndoa tena ila tu ikiwa wao wenyewe wanaona kufanya hivyo watakuwa na utulivu zaidi. ➡Na Ikiwa watakuwa na Watoto basi bila shaka watoto waliowazaa kwa ndoa hiyo kabla kusilimu watakuwa wanatambulika kama watoto halali. ➡Tofauti inaweza kuwepo ikiwa watoto hawatosalimu kama wazazi wao, na ikiwa ni hivyo, watoto hawatoweza kuwarithi wazazi wao wala kinyume chake. Na Allaah Anajua zaidi Imeandaliwa na *Imaam Masjid Tawbah*

Je, inafaa kwenda kwa mganga kwa lengo la kumrudisha Mume?

*Swali* Mume wangu amenikimbia yuko Mkoa mwingine na sipati huduma yeyote jee si dhambi kwenda kwa mganga ili apate kurudi? kama dhambi munanishauri nifanye nini na nasikia mtu akidai Talaka pepo ya Mola haisikii hata harufu?  Mtihani mkubwa kwangu umekuwa naomba msaada wenu. *Majibu* ✅Tambua na tahadhari kwamba kwenda kumkabili mganga ni kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Majina Yake na Sifa Zake tukufu kwani unamkabili mganga kwa kuamini kwamba yeye atakuwa na uwezo wa kumrudisha mume wako na hali yeye ni kiumbe kama wewe dhaifu kabisa. ⏩Waganga hawana ila kutumia uchawi na kulaghai watu kwa kutaka mapato au chumo kutoka kwa watu wanaomwendea. ➡Mtu Mwenye kumwendea mganga ikiwa kwa ajili ya kumtegemea amtatulie matatizo yake au amtabirie jambo, hutoka nje ya Uislamu kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)⤵ ((من أتى كاهناً فصدقه بما يقول فقد كفر بما أنزل على محمد صلى الله عليه وسلم))  رواه أبو داود   ((Atakayemwendea mcha

Fadhila za Kumswalia Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi Sallaam)

*Fadhila za Kumswalia Mtume Muhammad (Swallaah Allahu Aleyhi wa Sallaam)* ➡Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema⤵ إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Nabiy. Enyi walioamini mswalieni na msalimieni kwa maamkizi ya amani na kwa tasliymaa.  ↪Surat Al-Ahzaab Aya ya 56. ✅Maana ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): *Ni kumsifia kwa Malaika, kumteremshia rahmah na baraka, fadhila nakadhalika.* ✅Maana ya Malaika Wake kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kumuombea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  *du’aa Amghufurie na Amteremshie baraka.*  ✅Maana ya Waumini kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni *kumuombea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) du’aa na amani.* ➡Juu ya hivyo Waumini kumswalia M