Kufupisha kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Mfumo wowote Haijuzu
Kufupisha kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Mfumo wowote Haijuzu Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amejibu kuhusu swali la hukmu ya kufupisha kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Kama ilivyoamrishwa kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwenye Swalaah katika Tashahhud, na imeamrishwa katika kutoa khutbah na kuomba Du’aa na kuomba maghfirah, na baada ya Adhaan, na wakati wa kuingia na kutoka Msikitini, na wakati wa kumtaja katika hali nyinginezo, hivyo basi ni muhimu zaidi kufanya hivyo katika kumtaja jina lake katika kitabu, barua, makala n.k. Kwa hiyo, imeamrishwa kuandika Swalaah na Salaam kwa ukamilifu ili kutimiza amri ya Allaah ('Azza wa Jalla) Aliyotuamrisha na ili msomaji apate kukumbuka kutaja kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapoisoma. Hivyo tusiandike Swalaah na Salaam kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aa