Neema za Pepo Tuliyoahidiwa Maelezo ya Neema za Pepo tuliyoahidiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) yametajwa mno katika Qur-aan na Hadiyth, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala): إنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا . حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا. وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا. وَكَأْسًا دِهَاقًا. لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا جَزَاء مِّن رَّبِّكَ عَطَاء حِسَابًا. ((Hakika wenye taqwa [wamchao Allaah] wanastahiki kufuzu. Mabustani na mizabibu. Na wake waliolingana nao. Na bilauri zilizojaa. Hawatosikia humo upuuzi wala uongo. Malipo kutoka kwa Mola wako kipawa cha kutosha)) [An-Nabaa: 31-36] Anasema tena (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Suratul-Waaqiah وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ. أُوْلَئِكَ الْمُقَرَّبُونَ. فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ. ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ. وَقَلِيلٌ مِّنَ الْآخِرِينَ. عَلَى سُرُرٍ مَّوْضُونَةٍ. مُتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq