Kisa cha Ummu Haraam Bint Milhaan ( Radhwiya Allaahu 'Anhum ) Na Ustadh Arabi Ibn Saidi Haraam bin Milhaan na Sulaym bin Milhaan pamoja na dada zao Ummu Haraam bint Milhaan na Ummu Sulaym bint Milhaan (Radhwiya Allaahu 'anhum) ni ndugu wanne waliosilimu wote kwa pamoja tena siku moja mara baada ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwasili mji wa Madyinah. Ndugu hawa walikuwa wakipendana sana na walikuwa wakimpenda sana Allaah na wakimpenda Rasuli Wake Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na wote kwa pamoja walikuwa na shauku kubwa ya kufa kifo cha shaahid kwa ajili ya kupata ushindi wa kuingizwa katika Pepo ya Mola wao Subhaanahu wa Ta'aalaa. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwapenda sana watu wa nyumba hii, na imepokelewa kuwa mara nyingi alikuwa akiwatembelea wakati wa mchana, akila na kuswali kwao swala za Sunnah. Ndugu wa kike walipewa majina ya kubandika (kun-yah), wakaitw
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq