Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Baada ya Allaah Kufaradhisha kufunga Ramadhaan, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawashaji´isha kuifuatisha Ramadhaan kwa kufunga siku zile za Shawwaal. Amefanya hivi ili ujira wao uweze kuwa mkubwa na ili waweze kulipwa kama aliyefunga mwaka mzima. Abu Ayyuub al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Anayefunga Ramadhaan na akaifuatisha kwa kufunga siku sita za Shawwaal, ni kama amefunga mwaka mzima.” Haafidhw al-Mundhiriy amesema: “ Ameipokea Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy, Ibn Maajah na at-Twabaraaniy amezidisha na kusema: “Nilisema: “Kila siku hulipwa kwa kumi.” Akasema: “Ndio.” Wamepokezi wake ni wapokezi sahihi. Mwaka hauwezi kuzidi siku 360. Siku sita za Shawwaal zikiwekwa katika Ramadhaan nzima na kila siku moja inalipwa kwa thawabu kumi (kwa kuwa tendo moja zuri linalipwa mara kumi) Waislamu wanazingatiwa kuwa wame
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq