SWALI: Assalam aleikum warahma tullahi wabarakatu Kutoka katika hadith Qudsi Allah amesema, Mtu yeyote atakaye sema: Astagh'firullah dhul jalali wal- ikramu min jamii dhunubi wal-aatham" mara 1000 katika mwezi wa Rajab basi sitomuadhibu mtu huyo katika kaburi wala siku ya kiama watumie Waislam wengine. JIBU: AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. Hakuna dalili ya fadhila hizo. Baada ya utafiti tumetambua kwamba uzushi wa du’aa na adhkaar kama hizo zimejaa katika vitabu na mitandao ya Kishia. Uzushi huo unasambazwa katika mitandao ya jamiii na la kusikitisha ni kuona jinsi Waislamu wanavyoharakisha kuwatumia watu bila ya kufanya utafiti, kwa kutekeleza amri ya mzushi huyo katika hilo swali hapo juu kuwa ‘watumie Waislam wengi
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq