Ni Sunnah kuswali Rak´ah mbili baada ya ´Aswr Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haachi Rak´ah mbili kabla ya Fajr na Rak´ah mbili baada ya ´Aswr. Ameipokea Ibn Abiy Shaybah katika ”al-Muswannaf” (2/352): ´Affaan ametuhadithia: Abu ´Awaanah ametuhadithia: Ibraahiym bin Muhammad bin al-Muntashir ametuhadithia, kutoka kwa baba yangu ambaye alikuwa akiswali Rak´ah mbili baada ya ´Aswr. Wakati alipoulizwa akasema: ”Nisingeziswali isipokuwa ni kwa sababu nilimuona Masruuq akiziswali, pamoja na kwamba alikuwa ni mtu mwaminifu. Lakini nikamuuliza ´Aaishah kuhusu jambo hilo ambapo akasema: ”Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haachi Rak´ah mbili kabla ya Fajr na Rak´ah mbili baada ya ´Aswr.” Miongoni mwa makosa yaliyoenea katika vitabu vya Fiqh ni pale wanapokataza Rak´ah mbili hizi bali na kutozitaja miongoni mwa jumla ya Sunnah za Rawaatib, pamoja na kwamba zimethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akidumu kwazo kama ambavyo alikuwa akidumu kusw
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq