Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh (Watu wengi katika jamii wana mazoea baada ya kumaliza kusoma Qur-aan, kusema ‘Swadaqa Allaahu Al-‘Adhwiym’. Wengi wakiwa wameathirika kwa mazoea ima ya kusikia kwenye radio au ya kuona video mbalimbali au Misikitini kutoka kwa wasomaji Qur-aan mbalimbali walio mashuhuri. Ada hiyo, haina dalili yoyote katika shariy’ah. Bali ni kinyume na ilivyothibiti kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na waja wema waliotangulia). Baada ya kumaliza kusoma Qur-aan usiseme ‘Swadaqa Allaahu Al-‘Adhwiym’, lakini sema: سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ، أشهد أن لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْك “ Subhaanaka Allaahumma wa Bihamdika , Ash-hadu Allaa ilaaha illa Anta, Astaghfiruka wa Atuwbu ilayka .” Ni jambo la ki-Sunnah ambalo wanaghafilika nalo watu wengi baada ya kumaliza kusoma Qur-aan. Ushahidi juu ya hilo ni Hadiyth kutoka kwa mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anh
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq