*Swali* Jirani yangu aliniuliza kuhusu mama yangu aliye fariki kama nimemtolea sadaka baada ya kufa mimi nikamjibu sikutoa sadaka yoyote, isipokua mimi nijuavyo kama ana deni inabidi nimlipie ikiwa deni hilo ni kwa binaadamu au kwa Mwenyezi Mungu na kama aliweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga inabidi pia nimlipie kwa kufunga. Na zaidi na muombea dua yeye akanijibu haifai mtu akifiwa na mama yake inabidi amtolee sadaka ampelekee majuzuu na misahafu madrasa au msikitini sasa sijui uthibitisho wa hili. *Jibu* ✅Maiti ananufaika kwa yote yaliyopitishwa na sheria ya Kiislamu ima katika Kitabu cha Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) na kwa uongofu wa Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). ➡Imepokewa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Anapokufa mwanaadamu basi amali zake zote hukatika isipokuwa kwa mambo matatu: Sadaka ya kuendelea, au elimu yenye manufaa au mtoto mwema anayemuombea” ↪Imepokelewa
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq