Kila sifa njema inamstahikia Allaah Aliyetukuka Muumba wa ulimwengu na walimwengu wake, ambae Alituwafikisha kuukamilisha mwezi wa Ramadhaan kwa kufunga Swawm yake nyakati za mchana, kusimama visimamo nyakati za usiku, kuisoma Qur-aan iliyoteremsha ndani yake na kutekeleza kila tulilowafikishwa kulitekeleza kadiri ya uwezo wetu. Swalah na Salamu zimfikie kipenzi cha Waumini Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Sahaba zake kiraam (Radhiya Allaahu 'anhum) na kila anaewafuata kwa ihsaanmpaka Siku ya Mwisho. Masiku ya Ramadhaan yaliyotunukiwa kila aina ya neema na baraka ndio yamekwishapita mpito wa usiku na mchana, na ndio hivyo hivyo unavyopita umri wetu, leo tuko hai juu ya ardhi na kesho wafu ndani yake. Ndugu yangu katika iymaan, umemaliza Swawm ya Ramadhaan na yote yaliyoambatana na Ramadhaan, mambo ambayo utekelezaji wake ulitarajiwa uwe wenye Ikhlaasw : kwamba hapakusudiwi katika utekelezaji wa hicho kinachotekelezwa chochote kile isipokuwa W
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq