Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2018

Hukmu ya Ghiyba ( kusengenya )

  Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Maana ya Ghiybah: Kilugha:    Kila kilichokuwa hakipo mbele yako. Na imeitwa Ghiybah kwa kutokuweko anayetajwa wakati anapotajwa na wengine.  Kishariy’ah : Kumsengenya mtu asiyekuwepo kwa mambo ambayo atachukia kuyasikia. Na maana yake ametujulisha Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipowauliza Maswahaba: ((   أتدرون ما الغيبة؟))  قالوا: الله ورسوله أعلم؛ قال:   (( ذكرك أخاك بما   يكره  ...)) ((Je mnajua maana ya  Ghiybah?)) Wakasema: Allaah na Rasuli Wake wanajua. Akasema: ((Kumsema ndugu yako anayoyachukia …..))   [Al-Bukhaariy] Imaam An-Nawawiy amesema kuhusu Ghiybah: "Kumsema mtu nyuma yake kwa yale anayoyachukia." Akaendelea kusema: "Kumsema mtu kwa anayoyachukia ikiwa yanayohusu mwili wake, au Dini yake, au dunia yake, au nafsi yake, au umbile lake au tabia yake, au mali yake, au wazazi wake, a...