Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Maana ya An-Namiymah Ni kufitinisha, kwa maana kuchongeza kwa kuhamisha au kupeleka maneno baina ya watu ili kusababisha wachukiane. Mfano kumwambia mwenzio: "Fulani kakusengenya wewe kadhaa na kadhaa." Au, "Fulani anakuchukia wala hakupendi." Kufitinisha huku kunaweza kuwa ni kwa kutamka maneno, au kwa kuandika au hata kwa kuonyesha ishara. Inaweza kuwa ni kufitinisha kwa kumsingizia mtu au hata kama huyo mtu alisema kweli usemi huo haijuzi kufitinisha. Mtu kama huyu mwenye kufitinisha ni mwenye nyuso mbili anamkabili kila mmoja kwa uso mzuri kumbe hampendelei kheri, ni kama kinyonga anayebadilika rangi kwa hali anayojipendelea nafsi yake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuonya watu kama hawa kwa kusema: عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إِنْ شَرَّ النَّاسِ ذُو الْوَجْهَيْنِ الَّذِي يَأ...
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq