Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Mwezi wa Ramadhwaan unathibitishwaje kuonekana kwake?

Mwezi wa Ramadhwaan unathibitishwa kuonekana kwake na mtu mmoja mwenye kujulikana kwa ukweli na kumcha kwake  Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) au kwa kutimiza siku thelathini za mwezi wa Sha’abaan. Ibn ´Umar amesema watu walikuwa wakitafuta kuandama kwa mwezi. nikamjulisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) kuwa mimi nimeuona mwezi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akafunga na akaamrisha watu wafunge.”  [Hadiyth Swahiyh. Angalia Kitaab I’rwa al-Ghaliyl na. 908 na Imeripotiwa na Abu Daawuwd]. Ikiwa mwezi haukuandama, kwa sababu ya kufunikwa na mawingu au kwa sababu nyingine basi hapo mwezi wa Sha’abaan utatimizwa kwa siku thelathini kama alivyoripoti Abu Hurayrah katika Hadiyth iliyo hapo juu. Lakini mwezi wa Shawwaal unatangazwa kuonekana kwa mashahidi wawili.’ ´Abdur-Rahmaan bin Zayd bin Al-Khattwaab amesema: “Nilipokuwa nikikhutubia siku ambayo ni ya shaka (kama mwezi wa Ramadhwaan kama umekwisha ama la), nikasema: “Nilikaa na Maswahaba zake Mtume (S...

Kutekeleza ´Ibaadah ya Kufunga Mwezi wa Ramadhwaan

                                      Kutekeleza ´Ibaadah ya Kufunga Mwezi wa Ramadhwaan Kufunga mwezi wa Ramadhwaan ni moja katika nguzo za Dini yetu ya Kiislamu na moja katika mambo ya lazima yampasayo kila Muislamu. Allaah (Subhanahu wa Ta’ala) Anasema: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ “Enyi mlioamini! Mmeandikiwa Swawm kama ilivyoandikwa kwa wale ambao wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa.”  [Suwratul Baqarah 02: 183]. Baada ya Aayah hii Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema tena: شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلاَ يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْ...

Njia za Kuukaribisha vizuri Mwezi Mtukufu wa Ramadhwaan

Inatupasa tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kwa kutupa umri tukiwa katika Uislamu na Iymaan hadi kutufikisha tena kukaribia Mwezi mtukufu wa Ramadhwaan. Na hii ni fursa nyingine Anayotupa Allaah Ta’aala katika maisha yetu kushuhudia mwezi huu na kupata fadhila zake.    Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa):      ((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ))  (( أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ... ((Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa Swawm, kama waliyofaradhishiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allaah)) (([Mfunge] siku maalumu za kuhisabika….   [Al-Baqarah: 183-184] Hii ni neema ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Ambaye Ametujaalia kuwa na miezi iliyo bora kuliko miezi mingine au siku bora au masaa bora kuliko mengine, ambazo thawabu zake za mema yanayotendeka humo huwa ni zaidi ya nyakati nyingine. Mfano wake ni kama kunapokuwa ...

Haijuzu kutamka Niyah

Amesema Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu-Allaah):    Kutamka niyyah ni upungufu katika akili na  Dini.  Ama katika Dini kwa sababu ni bid’ah, na katika akili ni kwa sababu ni sawa na ambaye anataka kula chakula husema: “Nanuia kuweka mkono wangu katika chombo hiki kwa kutaka nichote humo tonge la chakula niweke mdomoni mwangu kisha nimeze ili nishibe.” Basi huu ni ujinga na upumbavu. [ Al-Fataawaa Al-Kubraa  (2/213)]

Fiqh ya Swawm ya Ramadhwaan kutoka Kitabu ;Al-Wajiyz Fiy Fiqhis-Sunnah Wal-Kitaabil;Aziyz

Fiqh ya Swawm ya Ramadhwaan kutoka Kitabu ;Al-Wajiyz Fiy Fiqhis-Sunnah Wal-Kitaabil;Aziyz Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Kufunga mwezi wa Ramadhwaan ni moja katika nguzo za Dini yetu ya Kiislamu na moja katika mambo ya lazima yampasayo kila Muislamu. Allaah (Subhanahu wa Ta’ala) Anasema: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ “Enyi mlioamini! Mmeandikiwa Swawm kama ilivyoandikwa kwa wale ambao wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa.”  [Suwratul Baqarah 02: 183]. Baada ya Aayah hii Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema tena: شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلاَ يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُواْ الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ اللّهَ عَل...

Mwezi wa Ramadhwaan Imeteremshwa Qur-aan - Jichumie Fadhila za Kusoma na Kuhifadhi Qur-aan

Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Ndugu Muislamu, jitahidi utekeleze ‘ibaadah hii adhimu kwa wingi ya kusoma na kuhifadhi Qur-aan kwa sababu fadhila na thawabu zake ni nyingi na ‘adhimu mno kama tunavozinukuu baadhi yake humu.   Pia jitahidi uweze kuhitimisha (kumaliza kuisoma) Qur-aan japo mara moja katika mwezi huu wa Ramadhwaan kwa sababu mwezi huu ni mwezi ulioteremshwa Qur-aan kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):        شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ ...