Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah سبحانه وتعالى

 ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ))
((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyokuwa wakiyachuma)) [Yaasiyn:65
]

Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika.
Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah سبحانه وتعالى Atawafunga midomo yao
na kuviamrisha viungo vizungumze:
 عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى الله عليه وسلم، فضحك حتى بدت نواجذه، ثم قال:  (( أتدرون مم أضحك؟)) قلنا: الله ورسوله أعلم. قال: ((من مجادلة العبد ربه يوم القيامة، يقول: رب : ألم تجرني من الظلم؟ فيقول: بلى. فيقول: لا أجيز علي إلا شاهدًا من نفسي.   فيقول كَفَى بِنَفْسِكَ الْيَوْمَ عَلَيْكَ  ، وبالكرام الكاتبين  شهودا. فيختم على فيه، ويُقال لأركانه: انطقي. فتنطق بعمله، ثم يخلى بينه وبين الكلام، فيقول: بُعدًا لَكُنَّ وسُحقًا، فعنكنَّ كنتُ أناضل))  مسلم والنسائي،.
Imetoka kwa Anas Bin Maalik ambaye alisema, "Tulikuwa na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akacheka mpaka magego yake yakaonekana, kisha akauliza: ((Je? Mnajua kwa nini nacheka?)). Tukasema: Allaah na Mjumbe wake Wanajua.  Akasema: ((([Nacheka] kwa sababu ya majadiliano wa mja na Mola wake Siku ya Qiyaamah, atasema, Ewe Mola wangu, hutonihifadhi na dhulma? (Allaah) Atasema: Bila shaka. Atasema:  Sitokubali  shahidi yeyote dhidi yangu isipokuwa  mwenyewe. (Allaah) Atasema:  Nafsi yako inakutosha leo kukuhisabu. Na watukufu wenye kuandika watakuwa mashahidi dhidi yako.  Kisha mdomo wake utazibwa na vitaambiwa viungo vyake: Sema! (Viungo) vitasema aliyoyafanya. Kisha ataachiwa aseme na atasema (kuviambia viungo vyake): Angamieni, kwani ilikuwa kwa ajili yenu nikigombania ))  [Muslim 4.2280 na An-Nasai  katika Al-Kubrah 6:508
]
Hadiyth nyingine:
 عن أبو موسى الأشعري، رضي الله عنه-: ((يُدعى المؤمن للحساب يوم القيامة، فَيَعْرضُ عليه رَبُّه عملَه فيما بينه وبينه، فيعترف فيقول: نعم أيْ رب، عملتُ عملتُ عملت. قال: فيغفر الله له ذنوبه، ويستره منها. قال: فما على الأرض خَليقة ترى من تلك الذنوب شيئًا، وتبدو حسناته، فَوَدَّ أن الناس كلهم يرونها، ويُدعى الكافر والمنافق للحساب، فَيَعرضُ رَبُّه عليه عمله، فيجحد وفيقول: أي رب، وعزتك لقد كتب علي هذا الملك ما لم أعمل. فيقول له الملك: أما عملت كذا، في يوم كذا، في مكان كذا؟ فيقول: لا وعزتك أيْ رب ما عملتُه. فإذا فعل ذلك خُتِم على فيه((. قال أبو موسى الأشعري: فإني أحسب أول ما ينطق منه الفخذ اليمنى، ثم تلا    الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ
Imetoka kwa Abu Musa Al-Ash'ariyyiرضي الله عنه kwamba: ((Mu'uumini ataitwa kuhesabiwa siku ya Qiyaamah, na Mola wake atamuonyesha amali zake,  baina yake na Mola wake Atakubali na kukiri kwa kusema: Ndio Mola, nimefanya hayo.  Kisha Allaah Atamsamehe madhambi yake na Kuyaficha wala hakuna kiumbe katika ardhi atakayeona  madhambi hayo, lakini vitendo vyake vyema vitaonekana na Atataka watu wote wavione. Kisha Kafiri na Munaafiq ataletwa hesabuni na Mola wake atamuonyesha vitendo na atakanusha kwa kusema: Ewe Mola, kwa Utukufu Wako, Malaika huyu ameandika vitendo ambavyo sikuvifanya. Malaika atasema kumwambia: Hukufanya kadha na kadha, siku kadha na kadha? Atasema: Kwa Utukufu wako sikufanya.  Atakaposema hivi, Allaah Atamziba mdomo wake)). Abu Musa Al-Ash'ariyyi رضي الله عنه kasema: nafikiri kiungo cha kwanza kuzungumza kitakuwa ni paja la kulia.  Kisha akasoma:
   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ))
((Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyo kuwa wakiyachuma)) [Imaam Ahmad]

Hivyo ndivyo viungo vya mwili vitakavyomchongea mtu muovu siku ya Qiyaama kwa vitendo viovu vyote alivyovitenda. Na ushahidi mwingine Ametutolea Allaah سبحانه وتعالى  katika aya hizi pia:
 ((وَيَوْمَ يُحْشَرُ أَعْدَاء اللَّهِ إِلَى النَّارِ فَهُمْ يُوزَعُونَ))
)) حَتَّى إِذَا مَا جَاؤُوهَا شَهِدَ عَلَيْهِمْ سَمْعُهُمْ وَأَبْصَارُهُمْ وَجُلُودُهُمْ بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ))
 ((وَقَالُوا لِجُلُودِهِمْ لِمَ شَهِدتُّمْ عَلَيْنَا قَالُوا أَنطَقَنَا اللَّهُ الَّذِي أَنطَقَ كُلَّ شَيْءٍ وَهُوَ خَلَقَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ))
 ((وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَنْ يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ اللَّهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ))
((Na siku watakapokusanywa maadui wa Allaah  kwenye Moto, nao wakigawanywa kwa makundi))
((Hata watakapoufikia Moto yatawashuhudia masikio yao, na macho yao na ngozi zao kwa waliyokuwa wakiyatenda))
((Na wao wataziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia? Nazo zitasema: Ametutamkisha Allaah  Ambaye Ametamkisha kila kitu! Na Yeye ndiye Aliyekuumbeni mara ya kwanza, na Kwake Yeye tu mtarejeshwa))
((Na hamkuwa wenye kujificha hata masikio yenu, na macho yenu, na ngozi zenu, zisikushuhudilieni. Lakini mlidhani kwamba Allaah Hayajui mengi katika mliyo kuwa mkiyatenda))[  Fus-swilat: 19-22]
Kwa hivyo inampasa Mwanaadamu ajichunge na maovu na atambue kuwa viungo alivyoumbwa navyo katika mwili wake ni kwa ajili ya matumizi yenye kumridhisha Mola wake, na sio kwa ajili ya ma'asi, kwani kila kiungo kitakuja kuulizwa:
 ((إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْؤُولا))

((Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitaulizwa)) [Al-Israa: 36]


Maana, mtu ataulizwa siku ya Qiyaama kuhusu hivyo viungo (alivyovitumia) na viungo vitaulizwa kuhusu yeye (Mtu) na ataulizwa kavitumia vipi. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...