Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Neema za Pepo tuliyoahidiwa

                                                           Neema za Pepo Tuliyoahidiwa



Maelezo ya Neema za Pepo tuliyoahidiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) yametajwa mno katika Qur-aan na Hadiyth, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

إنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا.  وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا. وَكَأْسًا دِهَاقًا. لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا جَزَاء مِّن رَّبِّكَ عَطَاء حِسَابًا. 

((Hakika wenye taqwa [wamchao Allaah] wanastahiki kufuzu. Mabustani na mizabibu. Na wake waliolingana nao. Na bilauri zilizojaa. Hawatosikia humo upuuzi wala uongo. Malipo kutoka kwa Mola wako kipawa cha kutosha)) [An-Nabaa: 31-36]


Anasema tena (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Suratul-Waaqiah

 وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ.  أُوْلَئِكَ الْمُقَرَّبُونَ.  فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ.  ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ.  وَقَلِيلٌ مِّنَ الْآخِرِينَ. عَلَى سُرُرٍ مَّوْضُونَةٍ. مُتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ. يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ.  بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ.  لَا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنزِفُونَ. وَفَاكِهَةٍ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ.  وَلَحْمِ طَيْرٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ. وَحُورٌ عِينٌ.  كَأَمْثَالِ اللُّؤْلُؤِ الْمَكْنُونِ.  جَزَاء بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ.

((Na wa mbele watakuwa mbele. Hao ndio watakaokaribishwa. Katika Bustani zenye neema. Fungu kubwa katika wa mwanzo. Na wachache katika wa mwisho. Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyotonewa. Wakiviegemea wakielekeana. Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele. Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi. Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa. Na matunda wayapendayo.Na nyama za ndege kama wanavyo tamani. Na Mahuurul-’Ayn.  Walio kama mfano wa lulu ziliohifadhiwa. Ni malipo kwa waliyokuwa wakiyatenda)) [Al-Waaqi’ah: 10-24]

Surah hiyo tukufu inaendelea kutaja Neema za Pepo

((لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا. إِلَّا قِيلًا سَلَامًا سَلَامًا. وَأَصْحَابُ الْيَمِينِ مَا أَصْحَابُ الْيَمِينِ. فِي سِدْرٍ مَّخْضُودٍ.  وَطَلْحٍ مَّنضُود. وَظِلٍّ مَّمْدُودٍ. وَمَاء مَّسْكُوبٍ. وَفَاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ.  لَّا مَقْطُوعَةٍ وَلَا مَمْنُوعَةٍ. وَفُرُشٍ مَّرْفُوعَةٍ. إِنَّا أَنشَأْنَاهُنَّ إِنشَاء. فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًاعُرُبًا أَتْرَابًا. لِّأَصْحَابِ الْيَمِينِ. ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ. وَثُلَّةٌ مِّنَ الْآخِرِينَ))

((Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi. Isipokuwa maneno ya Salama, Salama. Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani?  Katika mikunazi isiyo na miba.  Na migomba iliyopangiliwa. Na kivuli kilichotanda. Na maji yanayomiminika.  Na matunda mengi. Hayatindikii wala hayakatazwi. Na matandiko yaliyonyanyuliwa. Hakika Sisi Tutawaumba [Mahuurul-‘Ayn] upya. Na tutawafanya vijana. Wanapendana na waume zao, hirimu moja. Kwa ajili ya watu wa kuliani. Fungu kubwa katika wa mwanzo. Na fungu kubwa katika wa mwisho)) [Al-Waaqi’ah: 25-40]

Wa kwanza kuingia Peponi ni Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama alivyosema:

 (( آتي الجنةَ فأستفتحُ - أي فأستأذن - فيقولُ الخازنُ : من أنتَ ؟ فأقول : أنا محمد !! فيقول :بِكَ أُمرت ألا أفتحَ لأحدٍ قبلكَ (( أخرجه الإمام مسلم في صحيحه 

((Nitafika [katika mlango wa] Pepo nitaomba idhini ya kuingia, atasema milinzi: Nani wewe? Nitasema: Mimi ni Muhammad. Atasema: Kwako nimeamrishwa wala sikuamrishwa nimfungulie mtu mwingine kabla yako)) [Muslim]


Tutazame baadhi ya Hadiyth chache miongoni mwa nyingi  zinazosimulia neema za Pepo:

Daraja yake:
 
عن أبي سعيد الخدري عن النبي صلى الله عليه و سلم قال: ((إن في الجنة مئة درجة، ولو أن العالمين اجتمعوا في إحداهن وسعتهم)) رواه أحمد بن حنبل في مسنده

Kutoka kwa Abi Sa'iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika katika Pepo kuna daraja mia. Na lau kama walimwengu wangelikusanyika katika mojawapo wangeenea) [Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake]

عن أبي هريرة عن النبي صلى الله عليه و سلم قال: ((إن في الجنة مئة درجة أعدها الله للمجاهدين في سبيله، بين كل درجتين كما بين السماء و الأرض، فإذا سألتم الله فاسألوه الفردوس...إلخ)) رواه البخاري

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Katika Pepo kuna daraja mia ambazo Ameziahidi Allaah kwa wanaopigana Jihaad kwa ajili Yake, baina ya kila daraja mbili kama (masafa ya) baina mbingu na ardhi, kwa hivyo, mnapomuomba Allaah Mumuombe (pepo ya) Al-Firdaws))[al-Bukhaariy]


Hakuna uchafu humo

  قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إن أول زمرة يدخلون الجنة على صورة القمر ليلة البدر ، ثم الذين يلونهم على أشد كوكب دري في السماء إضاءة ، لا يبولون ولا يتغوطون ، ولا يتفلون ولا يمتخطون ، أمشاطهم الذهب ، ورشحهم المسك ، ومجامرهم الألوة - الألنجوج ، عود الطيب - وأزواجهم الحور العين ، على خلق رجل واحد ، على صورة أبيهم آدم ، ستون ذراعا في السماء((البخاري

Amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Kundi la mwanzo watakaongia Peponi watakuwa kama mwezi unapokuwa kamili. Kisha watafuatia ambao watakuwa kama nyota zinazong’ara mbinguni. Hawatakojoa, wala hawatofanya haja kubwa, wala  hawatotema mate, wala hawatopenga kamasi,  vitana vyao vya dhahabu na jasho lao litanukia kama  misk,  vyetezo vyao watatumia udi wa mawardi, wake zao watakuwa ni  Huurul-‘Ayn wenye macho makubwa. Watu watakuwa katika umbo la aina ya mtu mmoja, la baba yao Aadam [wakiwa] nchi sitini kwa urefu)) [Al-Bukhaariy]   


Mito yake

عَنْ حَكِيم بْن مُعَاوِيَة عَنْ أَبِيهِ قَالَ سَمِعْت رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُول: (( فِي الْجَنَّة بَحْر اللَّبَن وَبَحْر الْمَاء وَبَحْر الْعَسَل وَبَحْر الْخَمْر ثُمَّ تَشَقَّقُ الْأَنْهَار مِنْهَا بَعْد)) وَرَوَاهُ التِّرْمِذِيّ

Imetoka kwa Hakiym bin Mu'aawiyah kutoka kwa baba yake ambaye amesema: Nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Katika Pepo, kuna bahari ya maziwa, na bahari ya maji, na bahari ya asali na bahari ya ulevi [wenye ladha]) kisha mito itafunguka humo)) [At-Tirmidhiy]

Baada ya kutambua sifa chache hizo Pepo yenye Neema, tunatumai kwamba tutajitahdi kufanya mema mengi ili tujaaliwe kuingia Peponi ambako maisha yake ni ya kudumu milele kwa furaha na amani.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...