Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Aqiydah Iwe Mwanzo

Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh

 

Jambo la kwanza, kubwa, na la msingi katika kulingania watu kumtii Allaah, na kwa nini ‘Aqiydah iwe mwanzo.

 

‘Aqiydah ni lazima ije mwanzo kwa sababu, kinachozusha mgawanyiko na maangamizi katika ulimwengu wa Kiislamu ni kukosekana ‘Aqiydah iliyo sahihi.

 

 

Kwa Nini ‘Aqiydah Liwe Ni Jambo La Mwanzo?

 

Hakika ‘Aqiydah lazima ije mwanzo kwa sababu ni msingi wa Da’wah ya Mitume wote kama Allaah Alivotuma ujumbe Wake kupitia kwa Mitume Wake. Kama Anavyosema Allaah kwa kupitia kwa ulimi wa kila Mtume Aliyemtuma kwa watu wake:

“Enyi watu! Muabuduni Allaah, hamna mungu isipokuwa Yeye” (Surat Huud 11: 84)

 

‘Aqiydah lazima ije mwanzo kwa ajili ya kuepukana na kizuizi cha kubakia motoni (Jahannam) milele na kujiepusha na adhabu hiyo. Hamujasikia maneno ya Allaah Aliyetukuka:

“Hakika Allaah hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Allaah basi hakika amezua dhambi kubwa”

(Suratun Nisaa 4: 48)

 

Kumshirikisha Allaah ni dhambi kubwa ambayo inampelekea mja kutoka kwenye Tawhiyd (kumpwekesha Allaah), na Tawhiyd ni msingi wa usahihi wa ‘Aqiydah.

 

‘Aqiydah ni lazima iwe mwanzo vilevile kwa ajili kumshirikisha (Shirk) Allaah ni dhambi kubwa ambayo ni dalili ya madhara juu yetu kama Allaah Alivyosema:

“Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa” (Suratul Luqmaan 31:13)

‘Aqiydah ni lazima ije mwanzo kwa sababu, kinachozusha mgawanyiko na maangamizi katika ulimwengu wa Kiislamu ni kukosekana ‘Aqiydah iliyo sahihi na watu kufuata ‘Aqiydah zisizo sahihi.

 

Ndio maana ‘Aqiydah nyingi za Waislamu zimejaa ufisadi kwa mambo ambayo ni shirk kubwa kwa mfano utakuta watu wanatufu (wanazunguka) kwenye makaburi na kuwaomba maiti waliomo ndani ya makaburi hayo wawasaidie haja zao na kudhani kufanya hivyo watapata mahitaji yao na kukidhiwa shida zao.

Na kwa hali hiyo, watu kama hawa wamerudi nyuma kiwakati, wanajirudisha katika wakati wa Jaahilliyah (zama za ujinga kabla ya Uislamu).

Na wanajifanya kama hawajasikia maneno ya Allaah Aliyetukuka:
‘‘Mkiwaomba hawasikii maombi yenu; na hata wakisikia hawakujibuni. Na Siku ya Qiyaamah watakataa ushirikina wenu. Na hapana atakayekupa khabari vilivyo kama Yeye Mwenye khabari”

(Suurat Faatwir 35: 14)

 

Na sisi tunawakataza kufuata uzushi wa Masufi ambao wameweza kuueneza kwa watu wa kawaida wasio na elimu na hadi taqriban nchi mbalimbali zimekuwa zikiongozwa na kutawaliwa na uzushi wa hawa Masufi na bid’ah zao kama vile Mawlid.

Na hata uzushi wa aina mbalimbali kama kuwaiga Makafiri katika sherehe zao na sikukuu zao, achilia mbali uzushi mbalimbali wanaoufanya katika Dini ambao umegawa nchi zao na kuziweka mbali na Qur-aan na Sunnah.

 

Kwa haya machache ndugu yangu mpendwa, tumejaribu kuwaonyesha ukweli ya kwamba ‘Aqiydah ni jambo la muhimu na la mwanzo katika maisha yako na daima ‘Aqiydah inapaswa iwe mwanzo.

Na Allaah anajua zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...