Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Hukumu ya Kusema ‘''Swadaqa Allaahu Al-‘Adhwiym''’ baada ya Kusoma Qur-aan

Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh

(Watu wengi katika jamii wana mazoea baada ya kumaliza kusoma Qur-aan, kusema ‘Swadaqa Allaahu Al-‘Adhwiym’. Wengi wakiwa wameathirika kwa mazoea ima ya kusikia kwenye radio au ya kuona video mbalimbali au Misikitini kutoka kwa wasomaji Qur-aan mbalimbali walio mashuhuri.

 

Ada hiyo, haina dalili yoyote katika shariy’ah. Bali ni kinyume na ilivyothibiti kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na waja wema waliotangulia).

 

Baada ya kumaliza kusoma Qur-aan usiseme ‘Swadaqa Allaahu Al-‘Adhwiym’, lakini sema:

 

سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ، أشهد أن لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْك

Subhaanaka Allaahumma wa Bihamdika, Ash-hadu Allaa ilaaha illa Anta, Astaghfiruka wa Atuwbu ilayka.”

 

Ni jambo la ki-Sunnah ambalo wanaghafilika nalo watu wengi baada ya kumaliza kusoma Qur-aan.

 

Ushahidi juu ya hilo ni Hadiyth kutoka kwa mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) aliposema:

 

“Hajapatapo kukaa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kikao chochote na wala  hajawahi  kusoma  chochote  kwenye  Qur-aanna wala  hajaswali  Swalaah yoyote  ila  alikhitimisha  (alimalizia kikao hicho) kwa  maneno (fulani).

Nikasema:

“Ee Rasuli wa Allaah,  ninakuona hukai kikao chochote, wala humalizi kusoma Qur-aan, wala humalizi  kuswali  Swalaah yoyote  ila unakhitimisha (unamalizia) kwa kusema maneno hayo? 

 

Akasema (Rasuli Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

“Ndio, yeyote ambaye atasema khayr atakhitimishiwa khayr hiyo. Na ambaye atazungumza maovu basi maneno (haya) yatakuwa ni kafara kwake (kwa yale maovu aliyoyasema katika kikao chake hicho).

 

سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ، أشهد أن لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْك

Subhaanaka Allaahumma wa Bihamdika, Ash-hadu Allaa ilaaha illa Anta, Astaghfiruka wa Atuwbu ilayka.”

[Umetakasika Ee Rabb wangu, na Himidi  ni Zako, Nashuhudia kwa hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Nakuomba maghfirah na natubia Kwako.]

 

[Hadiyth hii Isnaad yake ni sahihi kaitoa Imaam An-Nasaaiy kwenye ‘Sunan Al-Kubraa.

 

Na amesema Al-Haafidhw Ibn Hajr katika ‘An-Nukat’, mj. 2, uk. 733, kuwa Isnaad yake ni sahihi.

 

Na amesema Imaam Al-Albaaniy katika ‘Silsilat Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah, mj. 7, uk. 495, kuwa Isnaad hii ni sahihi vilevile kwa sharti ya Imaam Muslim.

 

Na amesema Shaykh Muqbil Al-Waadi’iy katika ‘Al-Jaami’ Asw-Swahiyh Mimmaa Laysa Fiy Asw-Swahiyhayn, mj. 2, uk. 128, kuwa Hadiyth hii ni sahihi.

 

Imaam An-Nasaaiy kaikusanya Hadiyth hii kwenye Sunan yake na akaiwekea mlango aliouita, “Chenye (Maneno) Kukhitimishiwa Kisomo Cha Qur-aan.”

 

Hivyo basi, baada ya ushahidi huo juu, na kukosekana ushahidi wa yale yaliyozooleka na watu wengi, kusema ‘Swadaqa Allaahu Al-‘Adhwiym’ baada ya kumaliza kusoma Qur-aan ni bid’ah; jambo lililozushwa katika Dini, na hivyo, watu wajiepushe na matumizi ya neno hilo katika mahali hapo.

 

Na kulijaalia neno (Swadaqa Allaahu Al-‘Adhwiym) na mfano wake kuwa ndio la kukhitimishia  kisomo cha Qur-aan ni bid’ah (uzushi).

 

Kwa sababu haijathibiti kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba aliyasema hayo maneno baada ya kumaliza kisomo cha Qur-aan.  Na lau yangekuwa maneno hayo yapo kishariy'ah basi angeyasema mwisho wake ( wakati anapomaliza kusoma Qur-aan).

 

Na kwa hakika imethibiti kutoka kwake kwamba amesema: 

"Yeyote atakayezua katika jambo (Dini) letu, lile ambalo halimo humo, basi atarudishiwa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Wa bi-LLaahit-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

[Al-Lajnatu Ad-Daaimah Lil-Buhuwth Al-‘Ilmiyyah Wal-Iftaa [Fatwa Namba 7306]

Na Allaah anajua zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...