Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kufuga Ndevu


Kuachilia ndevu ni wajibu kwa wanaume kwa dalili zifuatazo:


1- Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kuziachilia. Amri hii ni ya lazima, kwani hakuna kiashirio chochote kinachoigeuza na kuipeleka katika usunnah. Na kati ya amri hizo ni neno lake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 خالفوا المشركين: وفروا اللحى، وأحفوا الشوارب
((Kuweni kinyume na washirikina; fugeni ndevu kwa wingi na punguzeni masharubu)) [Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy (5892) na Muslim (259)]


Na neno lake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 جزوا الشوارب، وأرخوا اللحى، خالفوا المجوس
((Kateni masharubu na ziachilieni ndevu; nendeni kinyume na wanaoabudu moto)) [Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Muslim (260)]


2- Ni kwamba kuzinyoa ni sawa na kujifananisha na makafiri kama inavyoonekana katika Hadiyth mbili zilizotangulia.


3- Ni kwamba kuzinyoa ni sawa na kuubadilisha Uumbaji wa Mwenyezi Mungu na kumtii Shaytwaan asemaye:

وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ ۚ  
…na nitawaamrisha watabadili maumbile ya Allaah.”  [An-Nisaa: 119]

4- Ni kwamba kuzinyoa ni sawa na kujifananisha na wanawake. Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake [Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy (5885) na At-Tirmidhiy (2935)]


Na kwa ajili hiyo, Shaykh wa Uislamu amesema:
“Na inaharamishwa kunyoa ndevu zake” [Kitabu cha “Al-Ikhtiyaaraat Al-Fiqhiyyah” cha ‘Alaau Ddiyn Al-Ba’aly (uk.10). Angalia pia kitabu cha“Al-Furu’u” cha Ibn Muflih (1/291).]

Ibn Hazm na wengineo, wamenukulu Ijmaa’ ya Maulamaa juu ya uharamu wa kunyoa ndevu.


Je, Inajuzu Kupunguza Ndevu Zilizozidi Mshiko Wa Kiganja?

Baadhi ya Maulamaa wamefuata mwelekeo wa kujuzu kuondosha ndevu zilizozidi mkamato wa kiganja. Wao wameshikilia Hadiyth ya Ibn ‘Umar ambaye wakati wa kuhiji au kufanya ‘Umrah, alikuwa akizikamata ndevu zake, kilichozidi alikuwa akikiondosha.

Wamesema: “Yeye ndiye mpokezi wa Hadiyth yenye kuamuru kuachilia ndevu kwa wingi, hivyo basi yeye ndiye ajuaye zaidi upokezi wake!

Katika kaulipokezi hii, wao hawana hoja yoyote kwa dalili zifuatazo:

1- Kwamba Ibn ‘Umar Allah Amridhie, alikuwa akifanya hivyo wakati anapojifungua na ihraam ya Hija au ‘Umrah, wakati wao (Maulamaa hao) wanalijuzisha hilo nyakati zote.


2- Kwamba kitendo hiki cha Ibn ‘Umar kimefahamika kutokana na yeye kuliawilisha neno Lake Subhaanah:
   مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمْ وَمُقَصِّرِينَ

… wenye kunyoa vichwa vyenu na wenye kupunguza, [Al-Fat-h: 27]

Katika ‘amali za Hijjah, kichwa hunyolewa na ndevu hupunguzwa.

3- Ni kwamba Swahaba akisema au kutenda kinyume na alivyohadithia, basi kinachozingatiwa ni maneno yake na wala si ufahamu wake wala kitendo chake. Kwani mazingatio ni kile kilichorufaishwa moja kwa moja kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

Na kutokana na yaliyotangulia, lililo sawa ni wajibu wa kuachia ndevu na kutozikata kwa kuutumia ujumuishi wa amri zilizokuja katika Hadiyth sahihi kama vile: (( Fugeni kwa wingi…, ziachilieni…, zifanyeni nyingi….)) kama walivyoeleka kwa hilo jamhuri ya Maulamaa. 



Na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...