Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mume kunyonya maziwa ya mkewe inafaa...?

Swali

Mume kunyonya maziwa (matiti) ya mkewe inafaa...?


Jibu


Hakuna Uharamu wa Mume  kunyonya matiti ya mke wake. 

Allaah(Subhaana wa Taala) Anasema kwamba: 

((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ وَاعْلَمُواْ أَنَّكُم مُّلاَقُوهُ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ))

((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Allaah , na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wape bishara njema Waumini)) [2:223]

Kwahiyo mwanamke anayo ruhusa ya kumchezea mkewe sehemu yoyote ya mwili wake pamoja na kunyonya maziwa ya mkewe isipokuwa tu Kufanya naye jimai kwa sehemu ya nyuma (liwati).

Aayah hii: Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. imeteremka kuhusu Mayahudi waliokuwa wakisema kuwa mwanaume akimuingilia mke wake kupitia upande wa nyuma basi anazaliwa mtoto akiwa ana makengeza. Ndipo ikateremka hii Aayah [Al-Bukhaariy, Muslim kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه)].

Pia, Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) alisema kuwa kauli hiyo; Wanawake zenu ni konde kwenu iliteremshwa kuhusu baadhi ya watu wa Answaar ambao walikuja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakamuuliza (kuhusu kumuingilia mwanamke kutokea upande wa nyuma) akawajibu: Muingilie vyovyote upendavyo madhali ni ukeni.”[Ahmad]


Hadiyth kama ilivyothibiti :
عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ يَهُودَ، كَانَتْ تَقُولُ إِذَا أُتِيَتِ الْمَرْأَةُ مِنْ دُبُرِهَا فِي قُبُلِهَا ثُمَّ حَمَلَتْ كَانَ وَلَدُهَا أَحْوَلَ ‏.‏ قَالَ فَأُنْزِلَتْ: ((نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ‏))
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah kwamba Mayahudi walikuwa wanasema pale mke anapoingiliwa mbele katika sehemu za siri, lakini akiwa amegeuka nyuma, na pindi anaposhika mimba husema kuwa mtoto atazaliwa kengeza. Hapo ikateremshwa Aayah:Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo.“  [Muslim Kitaab An-Nikaah]

Kwahiyo Mume inajuzu kwake kunyonya matiti ya mke wake.Na pia Mume hawi haramu kwake (kwa mkewe) hata kama atameza maziwa yake ya kifua.

Kwa maelezo zaidi Rejea Kitab Al-Lajnah ad-Daai´mah. al-Fataawaa al-Qayyimah lil-Usrah al-Muslimah, uk 118-119.


Na Allaah anajua zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Amana katika Uislamu

                                                   AMANA  KATIKA  UISLAMU Assallaaam Aleykum Sallaam WarahmatulLaah Wabarakatuh Baada ya kumhimidi na kumshukuru Allaah Aliyetukuka Ambaye Ametuneemesha na fursa hii ya kukutana ili kunasihiana na kukumbushana. Swalah na salamu zimfikiye hashimu, Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam), Maswahaba zake, ahli zake na Waumini wote mpaka Siku ya Qiyaamah. Maudhui yetu ya leo ni muhimu sana katika zama zetu za leo na matatizo mengi tunakumbana nayo kwa sababu ya kukosekana. Hiyo ni maudhui ya amana. Huenda mmoja wetu akauliza: Amana ina maana gani katika Dini yetu ya kweli? Suala hilo limejibiwa na Imaam al-Qurtwubiy (Allaah Amrehemu) pale aliposema: Amana inajumlisha shughuli zote za Kidini. Amana ndio faradhi ambazo kwayo Allaah Aliyetukuka Amewapatia waja Wake. Na wametofautiana katika tafsili, hivyo kukawa na kauli nyingi. Baadhi yake ni: Pakasemwa: Hiyo ni kuweka amana ya mali na nyengineyo.

Hukumu ya Mke kutoka nyumbani bila Ruksa ya mumewe

Naam shukrani kwa swali lako kuhusu mkeo kutoka bila ya ruhusa yako kwenda katika mishuari zake. Matatizo haya hutokea mara nyingi kwa mke kutokuwa na ufahamu na ujuzi wa Dini ya Kiislamu. Au mara nyingine huwa kweli ana elimu lakini hushindwa kufuata kimatendo kwa sababu moja au nyingine. Au huenda akawa na elimu, lakini akakosa Dini. Kwa ajili hiyo Imaam al-Bukhaariy, ana mlango katika  Swahiyh  yake wenye kichwa cha habari, “ Elimu Kabla Ya ‘Amali ”. Hata hivyo, huenda mtu akawa na elimu lakini akawa hana ‘amali kwa sababu ya kutokuwa na ikhlaasw.   Ni juu ya mke kumtii mumewe katika mambo yasiyo ya maasi, kwani hakuna utiifu katika maasiya. Ikiwa mume hakutoa ruhusa mbali na kuwa yu mbali na mkewe ni wajibu wa mke kutii amri hiyo. Hata hivyo, haifai kwa mume kuweka vikwazo vya kupita kiasi,  kama kumzuia kwenda kwa wazazi wake na mahali ambapo anaweza kupata elimu ya Kidini. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “ Wakikutiini, basi msiwatafutie njia ” (an-Nisaa’ [4]: 34). Hii