Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe
Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume.
Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa.
Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti yao ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah.
Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa.
Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi fulani ya kishirikina ambayo inakwenda kinyume na Uislamu na hapo shari’ah haitokubaliana nalo ikiwa ni hivyo.
Hivyo, inatakiwa uulize maana ya pesa kutiwa hapo ndani ya kitauna kisiwe cha rangi nyengine yoyote? Na kwanini yasitumwe mahari tu bila kuwekwa kwenye kitambaa?
Hivyo, ukipata majibu yako, basi utayalinganisha na hayo tuliyokueleza na utakuwa na jibu tayari kuhusiana na jambo hilo .
Na Allaah Anajua zaidi
Maoni