Anasema Allaah سبحانه وتعالى ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono yao , na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyokuwa wakiyachuma)) [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba". Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu". Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa, watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah سبحانه وتعالى Atawafunga midomo yao na kuviamrisha viungo vizungumze: عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...
Maoni