Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mwanamke Mja Mzito (Mwenye Mimba) au Mwenye Kunyonyesha

                              Mwanamke Mja Mzito (Mwenye Mimba) au Mwenye Kunyonyesha




Mwanamke mwenye mimba au mwenye kunyonyesha ambaye hana uwezo wa kufunga ama ambaye anahofia afya ya mtoto wake  anaweza asifunge, atalisha maskini mmoja na hawajibiki kuilipa siku aliyokula. Ibn ´Abbaas amesema:

“Ruhusa amepewa mtu mzima mume au mke ambapo wataoneleya tabu kufunga, hawatofunga ambapo hawatopendeleya kufunga na watalisha maskini mmoja kwa kila siku ya kufunga. Kisha hawatalipa siku walizokosa kufunga hii iliondolewa baada ya Aayah hii:

وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ
“Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. (kwa kila siku).” (Suuratul Baqarah 02 : 184)


Baada ya hapo ikahakikishwa  kuwa mtu mzima mume au mke ambao hawawezi kufunga  na mwanamke mwenye mimba au mwenye kunyonyesha, ikiwa watahofia, hawatafunga na watalisha maskini kwa kila siku ambayo hawakufunga. [Msururu wa Riwaayah hii ni madhubuti imeripotiwa na Al-Bayhaqiy]. Pia imerikodiwa kuwa alisema, ikiwa wakati wa Ramadhwaan mwanamke mwenye mimba anahofia afya yake, au mwenye kunyonyesha anahofia afya ya mtoto wake, hawatafunga na watalisha maskini mmoja kwa kila siku ambayo hawakufunga na hawatalipa siku hizo kwa kufunga. [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl mjallad 4 uk.19].

Nafi’iy alisema ‘’Mmoja katika mabanati wa Ibn ´Umar aliolewa na mwanamume wa ki-Quraysh. Akapata mimba na wakati wa Ramadhwaan anashikwa na kiu sana. Ibn ´Umar akamwambiya funguwa swawm yako na ulishe masikini kwa kila siku.’’[Msururu wa Riwaayah ni Swahiyh na Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl mjallad 4 uk.20. Imerikodiwa na ad-Daraqutniy].

Kiwango gani cha chakula anawajibika kulisha?

Imeelezwa kwamba Anas Ibn Malik alidhoofika sana na hakuweza kufunga mwaka mzima akatayarisha sufuriya THARIYD (Mkate na nyama uliolowana katika supu) kisha akaalika masikini thelathini akawalisha mpaka wakaridhika’’. [Msururu wa Riwaayah hii ni Swahiyh pia imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl, mjallad 4 uk.21 imerikodiwa na ad-Daraqutniy].

Na  Allaah  anajua  zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...