Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mambo yenye Umuhimu kwa Ujumla wa Kutekeleza ´Ibaadah ya Swawm (Kufunga)

              Mambo yenye Umuhimu kwa Ujumla wa Kutekeleza ´Ibaadah ya Swawm (Kufunga)



1. Niyyah.

Allaah (Subhanahu wa Ta’ala) Amesema:

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاء وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ وَذَلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ

“Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Allaah kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Swalah, na watoe Zakaah. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.” (Suuratul Bayyinah 98 : 05)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
’’Kila kitendo hulipwa (kutokana na) niyyah na kila mtu ni lili alilonuwiya.’’
Na niyyah mahala pake ni moyoni. Niyyah ya kufunga ni lazima iwe moyoni kila usiku kabla ya wakati wa Fajr kuingiya.
Hafsah (Radhiya Allaahu ´anha) amesema mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
‘’Hana swawm asiyenuwia kufunga kabla ya fajr.’’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh al-Jamiy´ as-Saghiyr, na.6238. Pia imerikodiwa na Abu Dawuud, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy].

2. Kujiepusha katika masiku ya kuamka na swawm na chochote chenye kubatilisha swawm yako (tangu wakati wa adhaana ya pili) na usiku mpaka kutakapopambauka (Jua kuchomoza).

Amesema Allaah (Subhanahu wa Ta’ala):

 وَكُلُواْ وَاشْرَبُواْ حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ثُمَّ أَتِمُّواْ الصِّيَامَ إِلَى الَّليْلِ

“Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni swawm mpaka usiku.” (Suuratul-Baqarah: 187).


Mambo Sita Yanayobatilisha Swawm
                                                                                               
         
1. na 2. Kula au kunywa kwa kukusudia.

3. Kujitapisha kusudi.

4. na 5. Mwanamke atakapopata ada yake mwezi akiwa katika swawm.

6. Kitendo cha Jimai.


Mambo Yaliyopendekezwa kwa Mwenye Kufunga

Imependekezwa kwa mwenye kufunga afuate Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) katika kujitayarisha na swawm yake nayo ni haya yafuatayo;

1. Kula daku

Amehadithia Anas (Radhiya Allaahu ´anhu) Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) amesema:

‘’Kuleni daku, kwani kula huko daku kuna baraka.” [Imeripotiwa na Imaam Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Nasaa’y na Ibn Maajah].

Na ‘’kuleni daku’’ hata kama kwa kunywa maji inatosheleza. ´Abdullaah Ibn ´Amr amehadithia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
’’Kuleni daku japo kwa kunwa tama la maji.’’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh al-Jamiy´ as-Swaghiyr na.2945 imeripotiwa na Ibn Hibbaan].

Pia Imependekezwa kuchelewesha kula daku. Amehadithiya Anas kutoka kwa Zayd ibn Thabit ambaye amesema:

‘’Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alikula daku kisha akatoka kwenda kuswali. Anas akamuuliza “Kulikuwa na muda gani baina chakula cha daku na adhaana?” Akajibu: “Ilikuwa kiasi cha kusoma Aayah khamsini za Qur-aan".[Imeripotiwa na Imam Al-Bukhaariy na  Muslim].

Pia ameruhusiwa amalize chakula chake anaposikia Adhaana ya Fajr. Abu Hurayrah amehadithia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
“Endapo mmoja wenu atasikiya adhaana na mkononi mwake ana kinywaji, asirudishe kinywaji hicho mpaka aridhike nacho.’’[yaani anywe mpaka amalize haja yake].[Imesahihishwa na Shaykh al-Albaaniy katika al-Jami' as-Swaghiyr na.607].

2. Kujiepusha na maneno ya Upuuzi na mambo yasofaidisha Swawm yako.

Amehadithia Abu Hurayrah Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
’’Ikiwa mmoja wenu yuko ndani ya swawm ajiepushe na kitendo cha jimai na mabishano. Na kukitoka mmoja anataka kupigana nawe basi mwambiye ‘’Mimi Nimefunga’’.[Imeripotiwa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim na An-Nasaaiy]. Tena amehadithiya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
’’Yeyote ambaye hatowacha kusema uongo na kutenda kwa uongo basi Allaah (SubhanaHu wa Ta’ala) hana haja yake kwa kuwacha chakula chake na kinywaji chake’’.[Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika mukhtasar Swahiyh Al-Al-Bukhaariy na.921].

3. Kuwa na moyo kutoa na kujifunza Kusoma Qur-aan

Ibn ´Abbaas amesema: ’’Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alikuwa mwenye moyo wa kutoa mali katika watu wote na akifanya vizuri kabisa. Alikuwa akitoa zaidi katika mwezi wa Ramadhwaan anapoonana na Malaika wa Allaah Jibriyl (´alayhis-Salaam). Jibriyl anaonana naye kila usiku wa Ramadhwaan mpaka mwezi umalizike. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) atasoma naye Qur-aan. Anapoonana na Jibriyl, alikuwa na moyo zaidi wa kufanya mema kuliko kuifadisha swawm yake’’. [Imeripotiwa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim].

4. Kukimbilia (kuharakisha) kufungua swawm

Sahl Ibn Sa'd amehadithiya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
’’Watu watakuwa katika kheri endapo watakimbilia kufungua swawm zao’’.

5. Kufungua Swawm na yale yaliotajwa katika Hadiyth ikiwa ni rahisi kufanya hivo.

Anas amehadithia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alikuwa akifunguwa swawm yake na Tende zilioiva kabla kusali. Kama si zilioiva alikuwa akifungua na Tende kavu. Kama hiyo pia haikupatikana basi alikuwa akifunguwa na kinywaji cha maji. [Ni Hadiyth Hasan Swahiyh katika al-Jamiy´ as-Swaghiyr na.2065]


Na  Allaah  anajua  zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...