Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye Muziki na Vinanda

Swali


Inafaa Kusikiliza Nasheed na Kaswida zenye  Muziki na Vinanda


Jibu 


Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu hukumu ya muziki inayotiwa katika Nashiyd na Qaswiydah.

Muziki na utumiaji wa ala za muziki ni haramu katika Dini yetu hii, Uislamu. Zifuatazo ni dalili kuhusu hilo:

 

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kutakuwa watu katika Ummah wangu watakao halalisha uzinzi, uvaaji wa Hariri, pombe (unywaji) na ma’aazif (ala za muziki)” (al-Bukhaariy).

 

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwisho wa zama (dunia) kutakuwa na maporomoko ya ardhi, mawe kutoka mbinguni na kugeuza kwa wanyama, wakati ambapo ala za muziki na waimbaji wanawake watakapoenea na pombe kuruhusiwa” (atw-Twabaraniy).

 

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Watu katika ummah wangu watakunywa pombe, kuiita kwa jina jingine. Watatiwa furaha kwa uchezaji wa ala za muziki na uimbaji wa wanawake (watakao waimbia). Allaah Ataifanya ardhi kuwameza wote na kuwageuza kuwa nyani na nguruwe” (Ibn Maajah).

 

Na Allaah Aliyetukuka Amesema:

Na katika watu wako wanaokhitari maneno ya upuuzi ili wawapoteze watu na njia ya Allaah, pasipo wao kujua lolote, na wanaicheza shere hiyo njia ya Allaah. Basi hao watapata adhabu ifedheheshayo” (Luqmaan [31]: 6).

 

Ibn Jariyr atw-Twabariy katika Jaami‘ul Bayaan amesema kuwa rai ya mufasirina wa Qur-aan kuhusiana na maana ya ibara “Lahwal Hadiyth (maneno ya upuuzi)” inaweza kugawanywa katika aina tatu. Nazo ni:

 

1.     Uimbaji na kusikiliza nyimbo.

2.     Kuajiri au kununua waimbaji wataalamu, wanaume na wanawake.

3.     Kununua ala za starehe.

 

Rai hii ndio iliyokuwa rai ya Maswahaba wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama Ibn Mas‘ud, Jaabir bin ‘Abdillaah na Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhum) {al-Kanadi Mustafa Abu Bilaal, The Islamic Ruling on Music and Singing in the Light of the Qur’an, Sunnah and the Consensus of the Salaf (Hukumu ya Kiislamu ya Muziki na Nyimbo katika Muono wa Qur-aan, Sunnah na Ijmaa ya Watangu Wema, uk. 9}.

 

Na pale Ibn Mas‘ud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipoulizwa kuhusu Aayah hii, alijibu: “Naapa kwa Yule ambaye hakuna Mola ila Yeye kuwa Aayah hii inamaanisha muziki”. Naye aliikariri ibara hiyo mara tatu kuitilia mkazo rai yake hiyo. Na waliokuwa na rai hiyo katika Tabi‘iyn ni ‘Ikrimah, Mujaahid, Makhuul, ‘Umar bin Shu‘ayb na wengineo.

 

Hata hivyo, upo wakati ambao mashairi yanaruhusiwa kuimbwa bila ya kuwepo kwa ala za muziki isipokuwa daff (dufu, twari) tu kwa wanawake. Na hali hizo ni kama:

 

1.   Wakati wa Jihaad na mapambano mengine katika Njia ya Allaah Aliyetukuka. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiimba wakati wa Vita vya Khandaq (Muslim).

 

2.   Wakati wa sherehe za Kiislamu kama ‘Iyd al-Fitwr na ‘Iyd Al-Adhwhaa.

 

3.   Pia ruhusa imetolewa kwa wanawake na wasichana kuimba na kupiga daff (dufu) wakati wa harusi.

Na Allaah anajua zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Mume kunyonya maziwa ya mkewe inafaa...?

Swali Mume kunyonya maziwa (matiti) ya mkewe inafaa...? Jibu Hakuna Uharamu wa Mume  kunyonya matiti ya mke wake.  Allaah(Subhaana wa Taala) Anasema kwamba:  ((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ وَاعْلَمُواْ أَنَّكُم مُّلاَقُوهُ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ)) ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Allaah , na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wape bishara njema Waumini)) [2:223] Kwahiyo mwanamke anayo ruhusa ya kumchezea mkewe sehemu yoyote ya mwili wake pamoja na kunyonya maziwa ya mkewe isipokuwa tu Kufanya naye jimai kwa sehemu ya nyuma (liwati). Aayah hii:  “ Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. “   imeteremka kuhusu Mayahudi waliokuwa wakisema kuwa mwanaume akimuingilia mke wake kupitia upande wa nyuma basi anazaliwa mtoto akiwa ana makengeza. Ndipo i

Amana katika Uislamu

                                                   AMANA  KATIKA  UISLAMU Assallaaam Aleykum Sallaam WarahmatulLaah Wabarakatuh Baada ya kumhimidi na kumshukuru Allaah Aliyetukuka Ambaye Ametuneemesha na fursa hii ya kukutana ili kunasihiana na kukumbushana. Swalah na salamu zimfikiye hashimu, Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam), Maswahaba zake, ahli zake na Waumini wote mpaka Siku ya Qiyaamah. Maudhui yetu ya leo ni muhimu sana katika zama zetu za leo na matatizo mengi tunakumbana nayo kwa sababu ya kukosekana. Hiyo ni maudhui ya amana. Huenda mmoja wetu akauliza: Amana ina maana gani katika Dini yetu ya kweli? Suala hilo limejibiwa na Imaam al-Qurtwubiy (Allaah Amrehemu) pale aliposema: Amana inajumlisha shughuli zote za Kidini. Amana ndio faradhi ambazo kwayo Allaah Aliyetukuka Amewapatia waja Wake. Na wametofautiana katika tafsili, hivyo kukawa na kauli nyingi. Baadhi yake ni: Pakasemwa: Hiyo ni kuweka amana ya mali na nyengineyo.