Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kupiga Mswaki Kwa Kutumia Dawa (Toothpaste) Kunabatilisha Swawm?

SWALI


Swali langu ni kama linavojieleza hapo juu kwenye kichwa cha hahari kuhusu kupiga mswaki kwa kutumia dawa ya colgate au dawa yeyote ile,kusema kweli hili suala limeulizwa na watu wengi sana na nyinyi mashehe zetu munalipeleka kwenye category ya kitu kinachobatilisha swaum, kwa maana hiyo hili suala halipo kabisa kwenye category hiyo, sasa tunakuombeni mtujibu hili tu ili tujue inafaa au laa.
Wabillahi Taufik,
Massalaam.


JIBU

Tunashukuru kwa Swali lako kuhusu kutumia dawa ya meno katika Swawm.


Hakuna makatazo ya kutumia dawa ya meno wakati unapiga mswaki ukiwa kwenye Swawm, ingawa kujiepusha kuitumia wakati wa Swawm ni bora ili usije kuimeza wakati unaitumia. 

Na vizuri  zaidi kutumia miswaak aliyokuwa akitumia Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam). Lakini ikiwa haikupatikana, na kuna haja ya kutumia dawa, basi hakuna neno kusafisha meno kwa dawa ya meno. 


Na kufanya hivyo hakubatilishi Swawm.  Lakini inapasa kuchukua tahadhari dawa isifike kooni na kuimeza ikabatilisha Swawm.     


Na Allaah Anajua zaid

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Mume kunyonya maziwa ya mkewe inafaa...?

Swali Mume kunyonya maziwa (matiti) ya mkewe inafaa...? Jibu Hakuna Uharamu wa Mume  kunyonya matiti ya mke wake.  Allaah(Subhaana wa Taala) Anasema kwamba:  ((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ وَاعْلَمُواْ أَنَّكُم مُّلاَقُوهُ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ)) ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Allaah , na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wape bishara njema Waumini)) [2:223] Kwahiyo mwanamke anayo ruhusa ya kumchezea mkewe sehemu yoyote ya mwili wake pamoja na kunyonya maziwa ya mkewe isipokuwa tu Kufanya naye jimai kwa sehemu ya nyuma (liwati). Aayah hii:  “ Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. “   imeteremka kuhusu Mayahudi waliokuwa wakisema kuwa mwanaume akimuingilia mke wake kupitia upande wa nyuma basi anazaliwa mtoto akiwa ana makengeza. Ndipo i

Amana katika Uislamu

                                                   AMANA  KATIKA  UISLAMU Assallaaam Aleykum Sallaam WarahmatulLaah Wabarakatuh Baada ya kumhimidi na kumshukuru Allaah Aliyetukuka Ambaye Ametuneemesha na fursa hii ya kukutana ili kunasihiana na kukumbushana. Swalah na salamu zimfikiye hashimu, Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam), Maswahaba zake, ahli zake na Waumini wote mpaka Siku ya Qiyaamah. Maudhui yetu ya leo ni muhimu sana katika zama zetu za leo na matatizo mengi tunakumbana nayo kwa sababu ya kukosekana. Hiyo ni maudhui ya amana. Huenda mmoja wetu akauliza: Amana ina maana gani katika Dini yetu ya kweli? Suala hilo limejibiwa na Imaam al-Qurtwubiy (Allaah Amrehemu) pale aliposema: Amana inajumlisha shughuli zote za Kidini. Amana ndio faradhi ambazo kwayo Allaah Aliyetukuka Amewapatia waja Wake. Na wametofautiana katika tafsili, hivyo kukawa na kauli nyingi. Baadhi yake ni: Pakasemwa: Hiyo ni kuweka amana ya mali na nyengineyo.

Hukumu ya Mke kutoka nyumbani bila Ruksa ya mumewe

Naam shukrani kwa swali lako kuhusu mkeo kutoka bila ya ruhusa yako kwenda katika mishuari zake. Matatizo haya hutokea mara nyingi kwa mke kutokuwa na ufahamu na ujuzi wa Dini ya Kiislamu. Au mara nyingine huwa kweli ana elimu lakini hushindwa kufuata kimatendo kwa sababu moja au nyingine. Au huenda akawa na elimu, lakini akakosa Dini. Kwa ajili hiyo Imaam al-Bukhaariy, ana mlango katika  Swahiyh  yake wenye kichwa cha habari, “ Elimu Kabla Ya ‘Amali ”. Hata hivyo, huenda mtu akawa na elimu lakini akawa hana ‘amali kwa sababu ya kutokuwa na ikhlaasw.   Ni juu ya mke kumtii mumewe katika mambo yasiyo ya maasi, kwani hakuna utiifu katika maasiya. Ikiwa mume hakutoa ruhusa mbali na kuwa yu mbali na mkewe ni wajibu wa mke kutii amri hiyo. Hata hivyo, haifai kwa mume kuweka vikwazo vya kupita kiasi,  kama kumzuia kwenda kwa wazazi wake na mahali ambapo anaweza kupata elimu ya Kidini. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “ Wakikutiini, basi msiwatafutie njia ” (an-Nisaa’ [4]: 34). Hii