Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Madhara Ya Ghiybah (Kusengenya) Na An-Namiymah (Kufitinisha) -Sehemu ya 3

Madhara Ya Ghiybah - Maana Ya Ghiybah, Tofauti Baina Ya Ghiybah, Buhtaan Na Ifk

 

Maana ya Ghiybah:

 

Kilugha:  Kila kilichokuwa hakipo mbele yako. Na imeitwa Ghiybah kwa kutokuweko anayetajwa wakati anapotajwa na wengine. 

 

Kishari’ah: Kumsengenya mtu asiyekuwepo kwa mambo ambayo atachukia kuyasikia. Na maana yake ametujulisha Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipowauliza Maswahaba:

 

(( أتدرون ما الغيبة؟))  قالوا: الله ورسوله أعلم؛ قال:(( ذكرك أخاك بما يكره  ...))

 

((Je mnajua maana ya Ghiybah? [Kusengenya])) Wakasema: Allaah na Mjumbe Wake wanajua. Akasema: ((Kumsema ndugu yako anayoyachukia …..)) [Al-Bukhaariy]
 

Imaam An-Nawawiy amesema kuhusu Ghiybah: "Kumsema mtu nyuma yake kwa yale anayoyachukia"

 

Akaendelea kusema: "Kumsema mtu kwa anayoyachukia ikiwa yanayohusu mwili wake, au dini yake, au dunia yake, au nafsi yake, au umbile lake au tabia yake, au mali yake, au wazazi wake, au mtoto wake, au mke wake, au mtumishi wake, au nguo yake, au nyendo (shughuli) zake na mengineyo yote yanayomhusu, ikiwa ni kumsema kwa kauli, au kwa ishara au kukonyeza, hata kama kusema neno la kumkejeli.

Maana nyingine ya Ghiybah ni kama alivyosema Ibn   Taymiyah: "Wengine wanasengenya kwa kauli zao za kustaajabu kama kusema: 'Nimeshangazwa na fulani vipi hafanyi kadhaa na kadhaa' na wengine wanaosengenya moyoni (kwa nia) kwa kunena: 'masikini fulani amenisikitisha anayoyatenda'

 

Tofauti Baina ya Ghiybah na Buhtaan

 

Buhtaan ni kumzulia mtu jambo lisilokuwa la kweli. Ametubainishia Mtume  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tofauti baina ya Ghiybah na Buhtaan katika Hadiyth ifuatayo:

  عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَال :  (( أَتَدْرُونَ مَا الْغِيبَةُ؟ ))  قَالُوا : اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ ، قَالَ  ((ذِكْرُكَأَخَاكَ بِمَا يَكْرَهُ )) ، قِيلَ : أَفَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ فِي أَخِي مَا أَقُولُ ؟ قَالَ  ((إِنْ كَانَ فِيهِ مَا تَقُولُ فَقَدِ اغْتَبْتَهُ ، وَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِيهِ فَقَدْ بَهَتَّهُ))    أخرجه مسلم  

 

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba aliuuliza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Je mnajua maana ya Ghiybah? [Kusengenya])) Wakasema: Allaah na Mjumbe Wake wanajua. Akasema: ((Ni kumtaja ndugu yako kwa jambo analochukia)). Akaulizwa: Hebu nieleze, iwapo ndugu yangu anayo yale niyasemayo? Akasema: (Ikiwa analo hilo usemalo basi umeshamsengenya, na ikiwa hana hilo usemalo basi umeshamzushia uongo)) [Muslim]

Vile vile Hadiyth ifuatayo inaelezea:

 

عبد الله بن عمرو أنهم ذكروا عند رسول الله صلى الله عليه وسلم رجلاً فقالوا: لا يأكل حتى يُطعم, ولا يَرحل حتى يُرحل, فقال النبي صلى الله عليه وسلم: ((اغتبتموه)) فقالوا: يا رسول الله: إنما حدثنا بما فيه قال: ((حسبك إذا ذكرت أخاك بما فيه))  المحدثالألباني  -  المصدر:السلسلة الصحيحة

 

Kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Amru kwamba walimtaja mtu mmoja mbele ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakasema: "Hali hadi alishwe, wala haendi hadi apelekwe" Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Mmemsengenya)). Wakasema: "Ewe Mjume wa Allaah, tumehadithia ya kweli aliyonayo" Akasema: ((Inakutosheleza kumsema ndugu yako kwa aliyonayo)) [Al-Albaaniy   katika Silsilatus-Swahiyhah]

 

 

 Na kutoka katika Qur-aan Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema::

 

((وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا))

 

((Na wale wanaowaudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilizo dhaahiri)) [Al-Ahzaab: 58]  

Vile vile katika kisa cha Ifk (kuzuliwa) Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) Anasema Allaah  (Subhaanahu wa Ta'ala):

 

 ((وَلَوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ قُلْتُم مَّا يَكُونُ لَنَا أَن نَّتَكَلَّمَ بِهَذَا سُبْحَانَكَ هَذَا بُهْتَانٌ عَظِيمٌ))

 

((Na kwa nini mlipoyasikia msiseme: Haitufalii kuzungumza haya. Subhaanak Umetakasika! Huu ni uzushi mkubwa!))[An-Nuur: 16]    

 

Uzushi unaweza kuwa kwa Ghiybah (kumsengenya nyuma yake mtu) au mbele yake. 

 

Hasan Al-Baswriy kasema: "Ghiybah ni tatu; zote zimo katika Qur-aan. Ghiybah(kusengenya) Ifk udaku/umbeya naBuhtaan (Uzushi).

Ama Ghiybah ni kumsengenya ndugu yako aliyo nayo, ama Ifk ni kusema unayoyasikia (umbeya) na ama Buhtaan ni kusingizia yasiyo kweli".

 
Mafunzo ya  mada hii yataendelea Insha Allaah kutaja madhara na adhabu za uovu huu ambao hakika ni dhambi kubwa zinazomharibia mtu amali zake asiweze kufaulu Peponi japokuwa ana ucha Mungu wa namna gani.

Inaendelea

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...