Madhara Ya Ghiybah - Kuharamisihwa Kwake Na Na Adhabu Zake Katika Sunnah
Baada ya kujikumbusha makatazo na adhabu za Ghiybah katika Qur-aan, tukaona jinsi gani maovu haya yalivyokemewa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), tunaendelea kutaja makatazo yake na adhabu zake katika Sunnah:
عن أبي بكرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال في خطبته يوم النحر بمنى في حجة الوداع: (( إن دمائكم، واموالكم وأعراضكم حرام عليكم كحرمة يومكم هذا، في شهركم هذا، في بلدكم هذا، ألا بلغت )) متفقعليه
Kutoka kwa Abu Bakrah (Radhiya Allaahu 'anhu) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema katika khutba yake ya siku ya An-Nahr [siku ya kuchinja – yaani siku ya 'Iydul-Adhwhaa] huko Minaa katika Hajjatulwadaa' [Hijjah ya kuaga] ((Hakika damu zenu, mali zenu na heshima zenu ni haramu kwenu kama uharamu (wa kutenda dhambi) siku yenu hii katika mji wenu huu. Je nimefikisha?))[Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth hii inatuonyesha jinsi gani makatazo hayo yaliyotajwa, yakiwemo ya kuvunjiana heshima yalivyokuwa mazito kwamba ni sawa na kutenda dhambi mji mtukufu na siku tukufu hiyo ya Yawmun-Nahr (siku ya kuchinja). Bila ya shaka kila mmoja wetu atapima umuhimu huu wa kuhifadhi heshima za wenzetu kwa kutowasengenya na kutoa aibu zao kwa wengine.
Ikiwa hata mtu ana sifa ambayo unaitaja nyuma yake huwa in maana ni kumsengenya kama alivyosema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), seuze iwe ni kumsengenya mtu kwa aibu asiyokuwa nayo au kumtolea aibu zake, au kumzulia kwa mabaya asiyokuwa nayo?
عن عائشة رضي الله عنها قالت: قلت للنبي صلى الله عليه وسلم حسبك من صفيه كذا وكذا. وقال بعض الرواة: تعني قصيرة، فقال: (( لقد قلت كلمة لو مزجت بماء البحر لمزجته )) قالت: وحكيت له إنسانا فقال: (( ما احب أني حكيت إنسانا وان لي كذا وكذا )) رواه أبو داود والترمذي وقال: حديث حسن صحيح.
Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) amesimulia: "Nilimwambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Achana na Swafiyyah; yuko kadhaa na kadhaa" yaani ni mfupi – Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hakika umetamka neno ambalo lau lingalichanganywa na maji ya bahari yangelibadilika)) (kutokana na uvundo wa neno hilo). 'Aaishah alisema: "Siku moja nilimuigiza mtu mbele yake Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: ((Mimi sipendi kumuiga mtu na ilhali mimi nina kadhaa na kadhaa)) [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth hii ni Hasan Sahiyh]
Dini yetu ya Kiislam imesisitiza sanakutunziana heshima na kuhifadhiana mabaya yetu.
عن عبد اللَّه بن عَمْرو بن الْعاص رضي اللَّهعنهما عن النَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : ((الْمُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ لِسانِهِ ويَدِهِ ، والْمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ ما نَهَى اللَّه عَنْهُ)) متفق عليه
Kutoka kwa 'Abdullaahi bin 'Amru bin Al-'Aasw (Radhiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muislam ni yule wanaosalimika Waislam kwa ulimi wake na mkono wake, na Muhaajir (mwenye kuhama) ni yule anayehama yale Aliyoyakataza Allaah )) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Umuhimu wa kuhifadhi ulimi ili usimuingize mtu motoni:
عن معاذِ بن جبلٍ رضي الله عنه قال: قلت: يا رسول الله، أخْبِرني بِعَمَلٍ يُدْخِلُني الجنَةَ ويُبَاعِدُني عَنِ النارِ. قال: ((لَقَدْ سألْتَ عَنْ عَظيمٍ، وإنَهُ لَيَسيرٌ عَلى من يَسَّرَهُ اللهُ تعالى عَلَيْهِ : تَعْبُدُ اللهَ لا تُشْرِكُ بِهِ شَيئاً، وتُقيمُ الصَّلاةَ ،وتُؤتي الزكاةَ، وتصومُ رمضانَ، وتَحُجُّ البيتَ))
.ثم قال: (( ألا أَدُلُّكَ على أبْوَابِ الخيرِ؟: الصَّومُ جُنَّةٌ، والصَّدقةُ تُطْفِىءُ الخَطِيئةَ كما يُطْفىءُ الماءُ النارَ، وصَلاةَ الرَّجُلِ في جَوْفِ الَّليْلِ، ثم تلا: ((تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنْ الْمَضَاجِعِ)) - حتى بلغ – ((يَعْمَلُونَ)) السجدة: 16-17 .
ثم قال: ((ألا أُخْبِرُكَ بِرَأسِ الأمْرِ وَعَمودِهِ وَذِرْوَةِ سَنَامِهِ؟)) قلتُ: بَلىَ يا رسول الله. قال: (( رَأْسُ الأمْرِ الإسلامُ، وعَمُودُهُ الصَّلاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الجِهادُ )).ثم قال: ((ألا أخْبِرُكَ بِمِلاكَ ذَلِكَ كلِّهِ ؟)) فَقُلْتُ بَلَى يا رَسول الله، فأخَذَ بِلِسانِهِ وقال: ((كُفَّ عَلَيْكَ هذا)) . قلت: يا نبيَّ الله، وإنَّا لمؤاخَذُونَ بِما نَتَكَلَّمُ بِه؟)) فقال: (( ثَكِلَتْكَ أمُّكَ يَا مُعَاذُ, وَهَلْ يَكُبُّ الناسَ في النارِ على وُجُوهِهِمْ )) أو قال: ((على مناخِرِهِم - إلاَّ حَصَائدُ ألسِنَتهم)) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
Kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Allaah! Niambie kitendo ambacho kitanipeleka peponi na kitaniokoa na moto. Akasema: ((Umeniuliza jambo kubwa lakini ni rahisi kwa yule ambaye Mola Amemsahilishia. Muabudu Allaah wala usimshirikishe na chochote, Swali, toa Zakaah, funga Ramadhaan, nenda kuhiji (Makka). Kisha akasema: ((Je? Nikuonyeshe milango ya kheri? Swawm ni ngao, Sadaka inazima dhambi kama vile maji yanavyozima moto, na kuswali katikati ya usiku: Kisha akasoma ((Mbavu zao zinaachana na vitanda….)) hadi ilipomalizikia Aayah ((…wanayoyatenda))[As-Sajdah 32 : 16 na 17]
Tena akasema: ((Je, nikwambie kilele chahilo jambo; nguzo yake na sehemu yake ya juu kabisa?)) Nikasema: Ndio ewe Mjumbe wa Allaah. Akasema: ((Kilele chake ni Uislam, nguzo yake ni Swalah na sehemu yake ya juu kabisa ni Jihaad)) Kisha akasema: ((Je, nikwambie muhimili wa yote haya?)) Nikasema: Ndio ewe Mjumbe wa Allaah. Akaukamata ulimi wake na akasema; ((Uzuie huu)) Nikasema: Ewe Mjumbe wa Allaah, yale tunayoyasema tutahukumiwa kwayo? Akasema: ((Mama yako akuhurumie ewe Mu'aadh! Kuna kitu zaidi kinachowaangusha watu kifudifudi motoni kama si mavuno ya ndimi zao?))[Imesimuliwa na At-Tirmidhiy na ni Hadiyth Hasan]
Baadhi ya hizo adhabu za Akhera alikwishaziona Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokwenda Israa wal Mi'raaj na katuelezea katika Hadiyth ifuatayo:
عن أنس قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم (( لما عرج بي مررت بقوم لهم أظفار من نحاس يخمشون وجوههم وصدورهم، فقلت: من هؤلاء يا جبريل؟)) قال: هؤلاء الذين يأكلون لحوم الناس ويقعون في أعراضهم"
Kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Nilipopandishwa mbinguni (Siku ya Israa na Mi’raaj) nilipita kwa watu ambao walikuwa wana kucha za shaba nyeupe wakijichana nyuso zao na vifua vyao. Nikauliza: Nani hawa ewe Jibriyl? Akasema: Hawa ni watu ambao wamekula nyama za binaadamu na kuwavunjia heshima zao)) [Abu Daawud]
Inaendelea
Maoni