Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Madhara Ya Ghiybah (Kusengenya) Na An-Namiymah (Kufitinisha) -,Sehemu ya 7

Madhara Ya Ghiybah - Vipi Kujiokoa Na Kuokoa Jamii Kutokana na Ghiybah

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

((وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّى يَخُوضُواْ فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلاَ تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَى مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ))  

((Na unapowaona wanaoziingilia Aayah zetu, basi jitenge nao mpaka waingilie mazungumzo mengine. Na kamaShaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kutanabahi usikae pamoja na watu madhaalimu)) [Al-An'aam: 68]

Hiyo ni moja ya njia ya kujiokoa na maovu haya ya Ghiybah, nayo ni kujiepusha na wanaopendelea kuzungumza yasiyo na maana na yanayomkosesha mtu radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Njia nyingine nyingi tunazitaja chini ya Makala hii na inayofuatia.

 

Njia Za Kujiokoa Na Kuwaokoa Wenzako Na Ghiybah:

1.     Kuwa na Taqwa na umkhofu Mola Wako na kusoma Aayah na Hadiyth zenye maonyo na adhabu za Ghiybah.

 

2.     Fikiria khasara utakayopata kumalizikiwa amali zako njema zote na kujazwa madhambi badala yake kama inavyosema Hadiyth ifuatayo:

‏ ‏عن ‏ ‏أبي هريرة رضي الله عنه ‏ ‏أن رسول الله ‏ ‏صلىالله عليه وسلم ‏ ‏قال‏‏)) أتدرون ما المفلس قالواالمفلس فينا يا رسول الله من لا درهم له ولا متاع قال رسول الله ‏ ‏صلى الله عليه وسلم ‏‏ المفلس من أمتي من يأتي يوم القيامة بصلاته وصيامه وزكاته ويأتي قد شتم هذا ‏ ‏وقذف ‏ ‏هذا وأكل مال هذا وسفك دم هذا وضرب هذا فيقعد ‏ ‏فيقتص ‏ ‏هذا من حسناته وهذا من حسناته فإن فنيت حسناته قبل أن ‏ ‏يقتص ‏ ‏ما عليه من الخطايا أخذ من خطاياهم فطرح عليه ثمطرح في النار)) ‏‏ا لترمذي

Imetoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mnamjua nani aliyefilisika?)) Wakasema (Maswahaba): Aliyefilisika ni yule miongoni mwetu asiyekuwa na Dirham au mali. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Aliyefilisika katika Ummah wangu ni yule atakayekuja siku ya Qiyaamah na Swalah zake, Swawm zake na Zakaah zake, lakini atakuja akiwa amemtukana huyu, amemtuhumu huyu, amekula mali ya huyu, amemwaga damu ya huyu na amempiga huyu, yatachukuliwa mema yake na kulipwa wale aliowadhulumu. Yatakapomalizika mema yake kabla ya kufidia madhambi aliyowakosea wenzake, zitachukuliwa dhambi za wale aliowakosea kisha atajaziwa yeye na mwishowe atakuwa niwa kutupwa motoni)) [At-Tirmidhiy]

3.                Fikiria aibu zako au aibu za ndugu, jamaa zako na uwaze kama utapenda aibu hizo zenu zidhihirike kwa wengine.

 

4.                Mshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa kukuepusha na aibu kama za wenzako na muombe Asikupe mtihani wa aibu kamahizo au nyinginezo.

 

5.                Jiepushe na watu waovu na vikao viovu na andamana na watu wema ambao watakuwa na mazungumzo ya kukupa faida badala ya kukuangamiza.

 

6.                Atakapokupigia simu mwenzio kutaka kusengenya, aidha muelezee wazi kuwa hutaki tena kusikia umbeya kwani unamkhofu Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), na umnasihi naye pia aache maouvu hayo kwa kumkumbusha adhabu zake. Anapokuanzia mfano, "Je umesikia habari ya fulani?" Mjibu: "Sijasikia na wala sitaki kusikia, tafadhali tuzungumze mengine". 

 

7.                Ikiwa huwezi kumuambia wazi wazi ingawa ni bora zaidi kufanya hivyo, basi kila anapotaka kumsengenya mtu, mfano anapokupigia simu jifanye una kazi na huna muda. Fanya hivyo siku ya kwanza, ya pili, ya tatu, endelea hatimaye atafahamu kuwa kumbe hutaki Ghiybah. Au anapokuanzia, babaisha kwa kumpa mazuri uliyojifunza ya dini, au maudhui yoyote nyingine ya kheri.

 

8.                Jipe adhabu mwenyewe kila unapomsengenya mtu kama walivyokuwa wakifanya Salafus-Swaalih (wema waliotangulia);

-Funga Swawm ya siku moja kila unapomsengenya mtu, hatimaye utashindwa kukaa na njaa kila siku.

-Toa kiasi fulani cha pesa kila unapomsengenya mtu iwe ni sadaka, utakapojiona unafilikisha utaacha kusengenya. 

 

9.                Hifadhi ulimi wako usizungumze ila mema tu, jifunze pole pole hata kwa kujikumbusha, mfano uweke kitu mdomonikama kijiwe au chembe ngumu isiyotafunika ili ibakie kukukumbusha kuzuia ulimi kusema yasiyo na maana.

 

10.           Jiepushe na moto pindi utakapolinda heshima ya mwenzio, kumbuka Hadiyth ifuatayo:

عن أبي الدرداء رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((من رد عرض أخيه رد الله عليه وجهه

من النار يوم القيامة)) رواه الترمذي وحسنه

Abu Ad-Dardaa (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: (Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayetetea heshima ya nduguye (Muislamu), Allaah Atamuepusha uso wake na moto)) [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth hii ni Hasan]

 

11.           Utakaposikia uzushi au mtu atakapomsengenya mwenziwe mbele yako sema kama Anavyotufunza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika kisa cha 'ifk'- uzushi wa kusingiziwa Mama wa Waumimi Bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha):

Kwanza: Jifikirie nafsi yako kama wewe pia unaweza kufanya maovu hayo yanayozungumzwa? Kwa hiyo dhana nzuri iwe pia kwa Waumini wenzako.

((لَوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ ظَنَّ الْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بِأَنفُسِهِمْ خَيْرًا وَقَالُوا هَذَا إِفْكٌ مُّبِينٌ))

((Kwa nini mliposikia khabari hii, wanaume Waumini na wanawake Waumini hawakuwadhania wenzao mema, na kusema: Huu ni uzushi dhaahiri?)) [An-Nuur: 12]

 

Pili: Kanusha kabisa uliyoyasikia nachukulia hayo kuwa ni uzushi na Mtukuze Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):   

((وَلَوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ قُلْتُم مَّا يَكُونُ لَنَا أَن نَّتَكَلَّمَ بِهَذَا سُبْحَانَكَ هَذَا بُهْتَانٌ عَظِيمٌ))

((Na kwa nini mlipoyasikia msiseme: Haitufalii kuzungumza haya. Subhaanak Umetakasika! Huu ni uzushi mkubwa!))[An-Nuur: 16]

Inaendelea

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...