Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Madhara Ya Ghiybah (Kusengenya) Na An-Namiymah (Kufitinisha) -Sehemu ya 6

Madhara Ya Ghiybah - Sababu Za Kutendeka Uovu Wa Ghiybah

 

1-Kuambatana na marafiki waovu  

 

 

Moja ya sababu inayosababisha kutenda maasi ya Ghiyba ni kuambatana na marafiki waovu wasiomkhofu Mola wao kwani rafiki muovu humuathiri mwenziwe kwa yale anayoyatenda. Mfano mzuri ametupigia  Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: (( إنما مثل الجليس الصالح و جليس السوء كحامل المسك ونافخ الكير، فحامل المسك إما أن يحذيك وإما أن تبتاع منه، وإما أن تجد منه ريحاً طيبة، ونافخ الكير إما أن يحرق ثيابك وإما أن تجد منه ريحاًخبيثة)) متفق عليه

 

 

Abu Muusa Al-Ash'ariyy (Radhiya Allaahu 'anhu) amesimulia: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mfano wa jaliys [mtu unayeambatana naye] mwema na jaliys mbaya ni kamamfano wa mbebaji miski na mfua chuma (anayevuvia kipulizo). Mbebaji miski ima atakupa au utanunua kutoka kwake au utapata harufu nzuri kwake. Na mfua chuma (anayepuliza kipulizo), ima atachoma nguo zako au utapata harufu mbaya kutoka kwake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

2-Kutokuzingatia aibu zake mwenyewe kwanza

 

Ghiybah ni maovu yanayopatikana katika kila jamii takriban. Hakika ni maradhi maovu kabisa yanayoleta madhara makubwa baina ya ndugu wa Kiislamu kwa kukashifiana na kutangaziana aibu zao. Tutambue kuwa hakuna binaadamu aliyekamilika, na kila mtu atakuwa na aibu zake kama si yeye mwenyewe binafsi basi ni katika familia yake, na kama si familia yake basi ni wa karibu yake n.k. Hata kama hakuna aibu yoyote kwake au kwa watu wake, basi akhofu kuwa huenda ikamfikia yeye aibu hiyo au ndugu zake au watoto wake au yeyote katika jamaa zake, hii imedhihirika sana kuwa ni malipo yanayowapata wanaopenda kusengenya wenzao, Allaah Huwalipa watu wa aina hiyo hapa hapa duniani kwa kuwafika aibu na mengineyo. 

 

 

 

 

3-Simu ni chanzo kikuu

 

 

Chanzo kikuu kinachofanikisha kutendeke Ghiybah na uzushi kuenea katika jamii kwa siku hizi, hasa katika nchi zilizoendelea ambako uchumi wao uko juu na gharama za mawasiliano ni rahisi mno na pia kuweko simu za bure ambazo kwa wengine huwa ndio kama chakula chao; huamka asubuhi na kitu cha kwanza ni kutafuta uzushi, umbeya na usengenyaji kwa mzushi kama yeye na kuanza kutangaza. Lau kama simu zingelikuwa ni za kulipiwa basi bila shaka wangelifilisika wenye kupenda kusengenya na kuzusha. Ama nchi nyingine ambako simu hulipiwa, pia nako uzushi unaenea kutokana na wepesi wa mawasiliano baina ya jamaa katika mikusanyiko mbali mbali ya kutembeleana au ya kishuguhuli za jamii na vikao vya mabarazani.

 

 

 

4-Kudhani kwamba kusikiliza tu hakuhusu kusengenya

 

 

Mara nyingi utamsikia mtu anasema: "Lakini mimi nasikiliza tu umbeya sitii langu". Mwenye kusema hivi atambue kuwa mwenye kusengenya na mwenye kusikia wote wako katika ushirikiano wa maovu haya. Na kila kiungo cha binaadamu kitamchongea mwenye kufanya maasi siku ya Qiyaamah, hivyo masikio yatakuchongea unaposikiliza umbeya au usengenyaji kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

((إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْؤُولاً))

 

 

((Hakika masikio, na macho, na moyo  hivyo vyote vitaulizwa)) [Al-Israa: 36]

 

 

 

5-Kujishughulisha na upuuzi badala ya kutumia muda kwa manufaa

 

 

 

Muda ni neema ambayo inampasa Muislamu ashukuru;  amejaaliwa kuwa yuhai, kwani kila dakika  ni muhimu kuitumia ipasavyo  kwa kujichumia mema na sio kuipoteza kwa mambo ya upuuzi khaswa yanayoweza kumuamgamiza mtu motoni kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

 

((فَوَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ))

  (( الَّذِينَ هُمْ فِي خَوْضٍ يَلْعَبُونَ))  

((Basi ole wao siku hiyo hao wanaokadhibisha))

 

 

((Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi)) [At-Twuur: 11-12]

 

Amesema Imaam Ibn Kathiyr: "Ni wale ambao duniani wanacheza katika mambo ya batili" Na kusengenya ni maovu, dhambi na batili inayompasa Muislamu ajiepushe nayo.

Inaendelea

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...