Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Madhara Ya Ghiybah (Kusengenya) Na An-Namiymah (Kufitinisha)

Madhara Ya An-Namiymah (Kufitinisha) - Sababu za Kufitinisha, Sifa Za Mfitinishaji -Sehemu ya 11

 

 

Kufitinisha baina ya watu ni jambo ovu linalochukiza mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ambaye Ametuamrisha tuepukane nalo kamaAnavyosema:

 

((وَتَعَاوَنُواْ عَلَى الْبرِّ وَالتَّقْوَى وَلاَ تَعَاوَنُواْ عَلَى الإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ))

 

((Na saidianeni katika wema na ucha Mungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui)) [Al-Maaidah :2]

 

 

Vile vile Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

 

 

((وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ))

 

((Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Allaah Hawapendi mafisadi)) [Al-Qaswas: 77]

 

Sababu zinazomfanya mtu afitinishe:

 

1.       Ujinga wa kutokujua makatazo yake katika Qur-aan na hatari yake na adhabu zake kutoka kwa Mola Muumba.

 

2.      Nafsi kuwa na chuki na uhasidi wa kuona ndugu wawili wanapendana na kushirikiana katika mambo yao. Amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عن أبي هُريرةَ رضي اللهُ عنه قال: قال رسوُل الله صلى الله عليه وسلم : ((لا تَحَاسَدُوا، ولا تَنَاجَشُوا، ولا تَباغَضُوا، ولا تَدَابَرُوا،  ولا يَبعْ بَعْضُكُمْ على  بَيْعِ بَعْضٍ، وكُونُوا عِبادَ اللهِ إخْوَاناً،  المُسْلمُ أَخُو المُسْلمِ: لا يَظْلِمُهُ، ولا يَكْذِبُهُ، ولا يَحْقِرُهُ، التَّقْوَى هاهُنا))  ويُشِيرُ إلى صَدْرِه  ثَلاثَ مَرَّاتٍ – ((بِحَسْبِ امْرِىءٍ مِنَ الشَّرِّ أن يَحْقِرَ أخاهُ المُسْلِمِ، كُلُّ المُسْلِمِ على الْمسْلِم حَرَامٌ:  دَمُهُ ومالُهُ وعِرْضُهُ")) رَوَاهُ مُسْلِمٌ   

 

 

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema:  Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Msioneane choyo, wala msizidishiane bei (za vitu), wala msichukiane, wala msipigane mapande (msitengane), wala msishindane kwa kupunguza bei.  Lakini kuweni ndugu, enyi waja wa Allaah, Muislamu ni ndugu wa Muislamu mwenzake, hamdhulumu wala hamvunji, hamwambii uongo wala hamdharau. Ucha Mungu  uko hapa (huku akiashiria kifuani kwa vidole vyake mara tatu) Ni uovu wa kutosha kwa mtu kumdharau ndugu yake Muislamu. Muislamu ameharamishiwa kwa Muislamu mwenzake: damu yake, maliyake na heshima yake [Yaani haramu kuchukua mali ya mwenzako, kumuua na kumdhalilisha] [Imesimuliwa na Muslim]  

 

 

 

3.     Kutaka kujikurubisha zaidi kwa mmoja wao aidha kwa kuona wivu kuwa wa kwanza hampendi kama anavyompenda wa pili.

 

 

4.     Kufuata maslahi yanayopatikana kwa mmoja wao ili afaidike naye baada ya kumfitinisha mwenzake.

 

Sifa za An-Nammaam (mwenye kufitinisha)

 

 

1.     Ni mwenye kupenda kuapa sana kwani hakuna mwenye kupenda kuapa sanaisipokuwa mtu asiye mkweli.  Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

 

((وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ)) (( هَمَّازٍ مَّشَّاء بِنَمِيمٍ)) 

 

((Wala usimtii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa)) ((Mtapitapi, apitaye akifitini)) [Al-Qalam: 10-11]

 

 

 

2.      Mwenye kupenda kusengenya na kuwatia aibu wenziwe aidha kwa kauli zake, au ishara wakiwa mbele yake au nyuma yake.

 

 

3.      Mwenye moyo mchafu usiopendelea kheri kwa wenzake.

 

 

4.      Huzidisha wema kwa wengine aonekane kuwa ni mwema, mwenye maneno mazuri. 

 

5.      Mwenye kupenda kulaumu bure bure almuradi tu akutie katika aibu kuwa una makosa japo atafute sababu yoyote imridhishe tu kuwa yeye ni mkweli na mwenziwe ni mkosa. 

Inaendelea

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...