Madhara Ya Ghiybah - Hali Zinazoruhusu Ghiybah
Tumebainishiwa katika Shari’ah yetu ya Kiislamu kuwa ziko hali zinazojuzu Ghiybah kwa sababu ya maslaha yanayopatikana. Nazo ni kama ifuatavyo:
1-Kupinga dhulma ya Qaadhi au Kiongozi au kuzuia dhulma isitendeke
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((لاَّ يُحِبُّ اللّهُ الْجَهْرَ بِالسُّوَءِ مِنَ الْقَوْلِ إِلاَّ مَن ظُلِمَ))
((Allaah Hapendi uovu uenezwe kwa maneno ila kwa mwenye kudhulumiwa))[An-Nisaa: 148].
2-Katika kushitaki anapodhulumiwa mtu haki yake:
Kutoa aibu ya mtu inapohitajika mfano kushtaki kwa mhusika (mkuu atakayeweza kutatua matatizo) kuwa 'fulani kanidhulumu kadhaa na kadhaa, au kanifanyia kadhaa na kadhaa, au fulani hanipi haki yangu kadhaa na kadhaa". Hii ni kutokana na dalili ya Hadiyth ifuatayo:
عن عائشة رضي الله عنها : أن هنداً زوجة أبي سفيان قالت : يارسول الله إن أبا سفيان رجل شحيح وليس يعطيني ما يكفيني وولدي إلا ما أخذت منه ، وهو لا يعلم ، فقال : ((خذي ما يكفيك وولدك بالمعروف)) متفق عيه
Kutoka kwa Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba Hind mke wa Abu Sufyaan alisema: "Ewe Mjumbe wa Allaah, Hakika Abu Sufyaan ni mtu bakhili, wala hanipi kinachonitosha mimi na mwanangu ila ninachokichukua ilihali hajui" (ni sawa hivi nifanyavyo?)" Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Chukua kwa wema kinachokutosha wewe na mwanao)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
3-Katika hali ya kubadilisha maovu
Huenda Muislamu akaona maovu yanatendeka na hatoweza kuyaondosha ila aulizie sababu, na huenda atakayeulizwa amseme aliyetenda maovu mfano 'fulani ndiye aliyefanya ovu hili kadhaa na kadhaa"
4-Kujikinga na shari, na kunapotolewa nasiha kwa Waislamu
عن فاطمة بنت قيس رضي الله عنها قالت أتيت النبي صلى الله عليه وسلم فقلت إن أبا الجهم ومعاوية خطباني فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم ((أما معاوية فصعلوك لا مال له وأما أبو الجهم فلا يضع العصا عن عاتقه)) متفق
وفي رواية لمسلم ((وأما أبو الجهم فضراب للنساء)) وهو تفسير لرواية لا يضع العصا عن عاتقه وقيل معناه كثير الأسفار
Faatwimah binti Qays (Radhiya Allaahu 'anha) amesimulia: "Nilimuendea Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikamuambia: "Abul-Jahmi na Mu'aawiyah wameniposa". Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: ((Ama Mu'aawiyah ni mtu fukara hanamali. Ama Abul-Jahmi haondoi fimbo juu ya shingo yake)) [Al-Bukhaaariy na Muslim]
Katika riwaaya nyingine ya Muslim imesema: ((Na ama Abul-Jahmi anawapiga mno wanawake))
Riwaaya hii ni tafsiyr ya riwaaya isemayo:((…haondoi fimbo juu ya shingo yake)) Na pia imesemekana kuwa maana ya kutoondosha fimbo juu ya shingo yake ni kuwa, anasafiri mno.
Ibnu Taymiyyah amesema: Huenda anapotajwa kwa ubaya mtu kukawa ni kwa ajili ya nasiha kwa Waislamu kwa usalama au manufaa ya Dini yao na dunia yao.
5-Kuwasengenya mafisadi na watu wenye shaka
Kama ilivyo katika Hadiyth ifuatayo ambayo Al-Bukhaairy ametoa hoja kuwa Hadiyth hii yafaa kuwasengenya wafisadi na watu wenye shaka.
عن عائشة رضي الله عنها أن رجلا استأذن على النبي صلى الله عليه وسلم فقال ((ائذنوا له بئس أخو العشيرة)) متفق
Kutoka kwa 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) amesimulia kuwa mtu mmoja aliomba idhini ya kuingia kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Mruhusuni, ni mtu mbaya katika kabila lake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
6-Kuihami Dini na wanafiki
عن عائشة رضي الله عنها قالت قال رسول اللهصلى الله عليه وسلم ((ما أظن فلانا وفلانا يعرفان من ديننا شيئا)) رواه البخاري
قال الليث بن سعد أحد رواة هذا الحديث هذان الرجلان كانا من المنافقين
Kutoka kwa 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Sidhani fulani na fulani wanajua chochote katika Dini yetu)) [Al-Bukhaariy]
Allayth bin Sa'ad ambaye ni mmoja wa wapokezi wa Hadiyth hii amesema: "Watu hawa wawili walikuwa ni katika wanafiki"
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala Atuhidi tuweze kutunza ndimi zetu ili tujiepushe hatari na dhambi za Ghiybah. Aamiyn
Inaendelea
Maoni