Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Ikiwa Majini Ni Viumbe Dhaifu Vipi Wamuingie Binaadamu Bila Ya Kuweza Kupona?

SWALI

 

Assalam alaykum warahmatul-allah wabarakatu.

 

Nimesikia kuwa majini ni viumbe dhaifu kuliko binaadamu na tunawaogopa bure tu, sasa suala langu linakuja pale tunapoona baadhi ya watu wanaugua maradhi ya mashetani (kupanda jini kichwani) baadhi ya walimu na masheikh wetu wanasema hakuna maradhi ya aina hii na mimi huko nyuma nimepata ku sikia kwamba, maradhi hayo yapo na yanatibika. Na kwa kusema hayo ni kutokana na mwalimu wangu kunipa hadithi ya kisa cha Nabii Sulaiman Bin daoud alokuwa Rasuli na Mfalme kwa viumbe vyote kwa wakati huo kwamba alipata kuwauliza majini kuhusu wanavyomuingia binaadam na kumpoteza au kumpatia maradhi na dawa gani itumike wao hutoka na wakampatia majibu kwa kumpa baadhi ya aya za Quran au sura kwamba zikisomwa hizi sisi hutoka na kumuacha huyo mtu. Jee lipi lina ukweli kati ya haya kuhusu maradhi hayo, yapo au hayapo, na kisa hiki ni sahihi au si sahihi?

 

Wabillah Tawfiq.

 

JIBU

Waleykum Salaam WarahmatulLaah Wabarakatuh

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukran zetu kwa swali lako kuhusu majini na mashaytwaan. Suala la majini kuwa ni dhaifu halina utata katika shariy'ah, kwani Allaah Aliyetukuka Anatuambia:

“Na hakika walikuwako wanaume katika watu waliokuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi” [72: 6].

 

Hiii hofu waliyokuwa nayo wanaadamu ndio iliyowafanya wao kuwaogopa majini na hivyo kuingia katika madhambi ya wazi.

 

Ama kuhusu mtu kuugua maradhi kwa kuingiwa na shaytwaan ni wazi kwani hata Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifanyiwa sihri na Myahudi, Labiyd mpaka Allaah Aliyetukuka Akawatuma Malaika kuja kumpatia ponyo na hivyo amri ya kusoma Mu’awwadhatayn (Surah ya 113 na 114) ili kumkinga yeye na huo uchawi. (al-Bukhaariy na Muslim).

 

Na hilo pia lipo wazi kabisa kama Anavyosema Allaah Aliyetukuka:

“Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Allaah. Na wanajifunza yatayowadhuru wala hayawanufaishi” (2: 102).

 

Kwa ajili ya kuwepo tatizo hili la mtu kukumbwa na jini au shaytwaan ndio Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatufunza njia za kujikinga na shari lao. Kwa kuwa maradhi hayo yapo bila shaka yana tiba kutoka katika Sunnah za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama yalivyopatikana katika vitabu vya Hadiyth.

 

Ama kuhusu kisa ulichotolewa na mwalimu wako kuwa tatizo hilo halipo, kisa hicho kina mashaka. Kisha kuna mgongano baina ya maelezo uliyoandika. Hebu tutazame yafuatayo:

 

Hicho kisa ni dalili kinyume na alivyotaka huyo mwalimu, kwani Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis Salaam) aliwauliza majini jinsi wanavyomuingia mtu au kumpatia maradhi.Kisha wakaulizwa majini kuhusu dawa nao wakatoa. Je, dawa hutolewa kwa asiye mgonjwa?Kuwa dawa aliyopatiwa Nabiy ni kisomo cha Qur-aan si sawa hata kimantiki kwani wakati huo Qur-aan ilikuwa haijateremshwa. Tufahamu kuwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja takriban miaka 1500 baada ya kuaga dunia Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis Salaam).

 

Hivyo, kisa cha mwalimu wako kinaunga mkono kuwa magonjwa hayo yapo. Na pia kurekebisha ibara uliyosema: “Nabii Sulaiman Bin daoud alokuwa Rasuli na Mfalme kwa viumbe vyote kwa wakati huo”, sio sawa kwani tunafahamu kuwa Manabiy wote walitumwa kwa watu wao isipokuwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye alitumwa kwa walimwengu wote. [Al-Bukhaariy na Muslim).

 

Kwa mukhtasari tunasema kuwa ugonjwa huo upo na una tiba yake kulingana na Sunnah za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...