Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
((يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ))
"Ee mwana Aadam! Nini kilichokughuri kuhusu Rabb wako Mkarimu?" [Al-Infitwaar: 6]
Utukufu gani wa Mwenye maneno haya yenye kushtua nyoyo na kusisimua mwili?Siku utakayoitwa "Ee Mwanaadamu maskini uliye dhaifu, kitu gani kikudanganyacho?"Nini kilichokughilibu hata ukamu'asi Allaah Mmoja (Pekee) Mwenye nguvu? (za mwisho)Nini kilichokudanganya hata ukavuka mipaka ya Mola wako?Nini kilichokudanganya hata ukapuuza Swalaah?Nini kilichokudanganya hata ukatenda maovu usiku na mchana?Nini kilichokudanganya hata ukapeleka macho yako kutazama yalio haramu?Nini kilichokudanganya hata ukawa humuogopi Mola wako kama unavyowaogopa viumbe vyengine?Nini kilichokudanganya hata ukawa huna khofu ya kukutana na Mola wako na kuhesabiwa?Je, ni dunia? Na Je? Hujui kama dunia ni nyumba ya kupita tu?Au ni shahawaat (matamanio)? Hujui kama nayo ni ya kuondoka?Au ni Shaytwaan aliyekuhadaa? Kwani hujui kama yeye kwako ni adui mkubwa?Basi ni kipi kilichokudanganya? Jibu! Jibu! Ndugu Muislamu, leo kabla ya kesho kufika! Kwani hujijui kama utafika kesho kama alivyosema Mshairi:
تزود من التقوى فإنك لا تدري
Zidisha taqwa kwani hujui
إذا جن عليك ليل هل تعيش إلى الفجر
Usiku utakapokufunika, je, utaishi hadi Alfajiri?
فكم من صحيح مات بغير علة
Kwani wangapi waliokuwa na siha zao wamekufa bila ya maradhi
وكم من سقيم عاش حينا من الدهري
Na wangapi walio wagonjwa wameishi miaka?
وكم من صغار يرتجى طولة عمرهم
Na Wangapi miongoni mwa wadogo wametumainiwa maisha marefu
وقد دخلت أجسادهم ظلمة القبر
Na miili yao imekwishaingia katika kiza cha kaburi
فكم من فتى يمسي ويصبح ضاحكا
Na vijana wangapi wameamka huku wanacheka
وقد نسجت أكفانه وهو لايدري
Kumbe huku sanda yao inashonwa/inaandaliwa naye hajui
وكم من عروس زينوها لزوجها
Na bi harusi wangapi amepambwa kwa ajili ya mume wake
وقد قبضت أرواحهم ليلة القدر
Na roho zao zimechukuliwa usiku wa Laylatul-Qadri?
وكم من ساكن عند الصباح بقصره
Na wangapi asubuhi walikuwa katika maqasri yao wakikaa
وعند المساء قد كان من ساكن القبر
Na jioni yakawa makazi yao ni kaburi?
فكن مخلصا وأعمل الخير دائما
Kuwa mwenye ikhlaas na utende mema daima
لعلك تحظى بالمثوبة والأجر
Huenda ukawafikishwa kupata thawabu na jazaa
وداوم على تقوى الإله فإنها أمان
Na dumisha Taqwa ya Mola Wa Pekee kwani ni hifadhi
من الأهوال في موقف الحشر
Itakayokulinda na hali katika siku ya kukufuliwa
لا إله إلا الله ...
Laa Ilaah Illa Allaah
Ee ndugu Muislamu imekuingia khofu ya kurudi kwa Mola wako na kuacha kuendelea kudanganyika?
Kumbuka madhambi yako na amka usiku ujikaribishe kwa Mola Mtukufu Mwenye kusamehe madhambi na Mwenye Rahmah na urudie hii Aayah mara kwa mara ili ingie katika moyo wako.
((يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ))
"Ee mwana Aadam! Nini kilichokughuri kuhusu Rabb wako Mkarimu?" [Al-Infitwaar: 6]
Ndugu Muislamu, tafakari matukio yaliyotajwa katika hii Surah Tukufu yatakayotokea siku ambayo hutoweza kujisaidia wala kusaidiwa!
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ ﴿١﴾
1. Mbingu zitakapopasuka.
وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انتَثَرَتْ ﴿٢﴾
2. Na sayari zitakapoanguka na kutawanyika.
وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ ﴿٣﴾
3. Na bahari zitakapolipuka.
وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ ﴿٤﴾
4. Na makaburi yatakapopinduliwa chini juu na kufichuliwa.
عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ﴿٥﴾
5. Nafsi itajua yale iliyoyakadimisha na iliyoyaakhirisha.
يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ ﴿٦﴾
6. Ee mwana Aadam! Nini kilichokughuri kuhusu Rabb wako Mkarimu?
الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ ﴿٧﴾
7. Ambaye Amekuumba Akakusawazisha (umbo sura, viungo) na Akakupima na kukulinganisha sawa.
فِي أَيِّ صُورَةٍ مَّا شَاءَ رَكَّبَكَ﴿٨﴾
8. Katika sura Aliyotaka Akakutengeneza.
[Al-Infitwaar: 1-8]
Maoni