Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kumpaka Mtoto Mchanga Wanja Au Masizi Usoni Kwa Ajili Kumkinga Na Husda Inafaa ?


SWALI:

 

Assalam Aleykoum Warrahmatullah Wabarakatu.

Suala langu la kumpaka mtoto mchanga wanja au masizi usoni ili iwe ni kinga kwa macho ya watu na husda ua kumvisha uzi mweusi ni kinga? na kama si kinga tumfanyie nini iwe kinga tumsomee ayatul kursi asubuhi na jioni au? Na kama nimefanya hivyo jee ni shirki? Naomba ufafanuzi haraka sana asanteni Mola akuzidishieni elmu na taqwa AMIN.

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumpaka mtoto mchanga wanja au masizi usoni kwa ajili ya kinga.

Hakika ni kuwa wanja ni dawa ya macho pekee wala si kinga ya hasadi. Kufanya hivyo, yaani kumpaka mtoto wanja au masizi usoni haifai kishari’ah kwani huko kunaingia katika shirki kwa kuufanya wanja na hayo masizi yanaweza yakamkinga mtoto.

 

Kinga ya mtoto ni kamaalivyotufundisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa tunaweza:

 

1.     Mume anapokutana na mkewe wawe watasoma du’aa: “Allaahumma jannibniy-sh Shaytwaana wa jannibish Shaytwaana maa razaqtana. Akiruzukiwa mtoto hatadhurika na Shaytwaan” (al-Bukhaariy).

 

2.     Kuwasomea watoto Suratul Ikhlaasw na kinga mbili (al-Falaq na an-Naas). Baada ya hapo kupuliza mkononi mwako na kuwapangusa mwili mzima.

 

 

3.     Na njia nyingine ni kuwasomea du’aa za kinga kama aliyofanya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa wajukuu zake: “U‘idhukumaa bikalimaatiLlaahi at-Taammaati min kulli Shaytwaaniw wa haammah wa min kulli ‘aynil laammah” (al-Bukhaariy)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...