Je, Damu Inazingatiwa Kuwa Ni Katika Najisi? Damu ina vigawanyo: 1- DAMU YA HEDHI : Damu hii ni najisi kwa makubaliano ya Maulamaa. Dalili ya unajisi wake imekwisha elezewa nyuma. 2- DAMU YA MWANADAMU [1] Ni damu iliyosababisha mahitalifiano juu ya hukumu yake. Lililo mashuhuri kwa watu wa madhehebu ya kifiqhi ni kwamba damu ni najisi, lakini wao hawana hoja. Isipokuwa damu imeharamishwa kwa matini ya Qur-aan katika neno Lake Aliyetukuka: ((قُل لاَّ أَجِدُ فِي مَا أُوْحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَى طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ ...
BismilLaahir Rahmanir Rahiim Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Blog hii ya www.fisabilillaah2011.blogspot.com Imeanzishwa na Arabi Saidi Mandota Mwaka 1437 H sawa na Mwaka 2017 M,kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Qur`an na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Wema Waliotangulia bila ya kujiegemeza katika kundi lolote lile. Wasiliana nami Whatssap namba +255 714 974 397 WabilLaah Tawfiq