Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Nani vipenzi vya Allaah..?


Nani Vipenzi Vya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)?

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

((أَلا إِنَّ أَوْلِيَاء اللّهِ لاَ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ))  ((الَّذِينَ آمَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ)) لَهُمُ الْبُشْرَى فِي الْحَياةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ لاَ تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللّهِ ذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ))  
((Tanabahi!  Hakika vipenzi wa Allaah hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.
 Ambao wameamini na wakawa wana taqwa.
 Watapata bishara katika uhai wa dunia na ya Aakhirah. Hakuna mabadiliko katika Maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu adhimu.))[Yuwnus: 62-64]

Aayah hizi tukufu zinataja 'Vipenzi Vya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Ni nani basi hao vipenzi Vyake Mola Mtukufu? Je, ndugu Muislamu, unamiliki sifa za kuwa ni waliyyu-Allaah? (kipenzi cha Allaah)?

Vipenzi vya Allaah ni kila aliyekuwa na sifa ya Aayah namba 63 nazo ni kuamini na kuwa na Taqwa, kwa maana kwamba wanafuata waliyoamrishwa na kujiepusha na waliyokatazwa.  

Huenda ikawa ni yeyote mmoja wenu madamu tu umetimiza sifa hizo basi umeshakuwa ni 'Walii Wa Allaah', na si kama wanavyodhani watu wengine kuwa ni watu makhsusi kama masharifu na mashekhe wala si watu wa kabila makhsusi au wenye kuvaa nguo makhsusi au kuishi mahali makhsusi.

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema kuwa  hao 'Awliyaa-Allaah' (Vipenzi vya Allaah) hawatokuwa na khofu wala hawatohuzunika.

Kama ilivyosemwa, kwamba huenda wakawa ni waja wowote na sio watu khaswa, wala wasiwe ni Mitume au Mashahidi kama alivyotujulisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):      
عن أبي هريرة، رضي الله عنه، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إن من عباد الله عبادا يغبطهم الأنبياء والشهداء)). قيل: من هم يا رسول الله؟ لعلنا نحبهم. قال: ((هم قوم تحابوا في الله من غير أموال ولا أنساب، وجوههم نور على منابر من نور، لا يخافون إذا خاف الناس، ولا يحزنون إذا حزن الناس)). ثم قرأ: (( أَلا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّهِ لا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلا هُمْ يَحْزَنُونَ ))  الطبري  ورواه النسائي  ورواه ابن حبان في صحيحه  
Imetoka kwa Abuu Hurayrah ((Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Miongoni mwa waja wa Allaah, watakuweko wale ambao Mitume na Mashahidi watawadhania kuwa ni wenye bahati)). Akaulizwa "Nani hao ewe Mjumbe wa Allaah ili tuwapende?" Akasema: ((Hawa ni watu waliopendana kwa ajili ya Allaah bila ya sababu ya maslahi ya kifedha au undugu (ujamaa), nyuso zao  zitaang'ara katika jukwaa la nuru. Hawatakuwa na khofu (siku hiyo) watakapokuwa na khofu watu wengine, wala hawatahuzunika watakapohuzunika watu wengine)). Kisha akasoma:((Sikiliezeni!  Vipenzi vya  Allaah hawatakuwa na khofu (siku ya Qiyaamah) wala hawatohuzunika))[Atw-Twabariy, Abuu Daawuwd, Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake]

Kisha Anaendelea Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  kusema:
((لَهُمُ الْبُشْرَى فِي الْحَياةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ لاَ تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللّهِ ذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ))
((Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Aakhirah. Hapana mabadiliko katika maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu kukubwa))[Yuwnus: 64]

Maana ya bishara njema katika maisha ya dunia na Aakhirah:
عن عبادة بن الصامت؛ أنه قرأ لرسول الله صلى الله عليه وسلم:(لَهُمُ الْبُشْرَى فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ) ثم قال: فقد عرفنا بشرى الآخرة الجنة، فما بشرى الدنيا؟ قال: ((الرؤيا الصالحة يراها العبد أو تُرَى له، وهي جزء من أربعة وأربعين جزءا أو سبعين جزءا من النبوة)).
'Ubaadah Bin Swaamit alimsomea Mtume:  ((Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Aakhirah)) kisha akasema: "Tunajua bishara ya Aakhirah kuwa ni Pepo, lakini nini bishara ya dunia?" Akasema (Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):  ((Ni ndoto njema (inayotokea kweli) anayoota mja au anayooteshwa. Ndoto hii ni sehemu moja kutoka sehemu arubaini na nne au sabiini za utume)) [Atw-Twabariy 15:132]

Vile vile imesemwa kuwa bishara njema ni ile anayoletewa Muumini na Malaika wakati wa mauti yake. Humletea bishara njema ya Pepo na maghfirah kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

((إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلائِكَةُ أَلا تَخَافُوا وَلا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنْتُمْ تُوعَدُونَ))
(( نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَةِ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنْفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ))
((نُزُلا مِنْ غَفُورٍ رَحِيم))  
((Hakika wale waliosema: “Rabb wetu ni Allaah.” Kisha wakathibitika imara; Malaika huwateremkia: (kuwaambia): “Msikhofu, na wala msihuzunike, na pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo mlikuwa mkiahidiwa.”
Sisi ni rafiki zenu walinzi katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Na mtapata humo yale yanayotamani nafsi zenu, na mtapata humo yale mtakayoomba.
Ni mapokezi ya takrima kutoka kwa Mwenye kughufuria, Mwenye kurehemu.)) [Fuswswilat: 30-32]


Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atujaalie ni katika Awliyaa Wake. Aamiyn.


www.fisabilillaah.blogspot.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe

                      Hukumu ya kupeleka barua ya posa kwenye kitambaa cheupe  Hakika ni kuwa posa ilivyofanyika katika Uislamu kuanzia wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafahamika vilivyo. Posa inaweza kuja kutoka kwa mume na watu wake kwa jamaa za mke au mzazi wa mke kumtafutia binti yake mume. Ikiwa wazazi watakwenda kwa wazazi wa mke, baada ya kupeleka maneno, na wazazi wa mke watataka kupatiwa muda wa kufikiria, kufanya shuuraa, kuulizia, kutafiti na baadaye kukubali au kukataa. Ikiwa wamekubali baada ya kumshauri binti  yao  ni vyema mume mtarajiwa aende amuone atakaye kuwa mkewe ili apate kutulia na kuridhika kabla siku ya Nikaah. Binti huyo au wazazi wake wataweka kiwango cha mahari ambacho mume anatakiwa kutoa. Hii njia ya kuweka pesa kwenye kitambaa au bahasha haipo katika mafunzo ya Kiislam, na huenda ni njia ya kitamaduni fulani au itikadi f...

Maana ya Uadilifu

                                         MAANA  YA  UADILIFU  KATIKA  UISLAMU Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd. Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Qur-aan. إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚيَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumb...

Viungo vya Mwili vitashuhudia Matendo ya Mwanaadamu Siku ya Qiyaamah

Anasema Allaah  سبحانه وتعالى   ((الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) ((Leo Tunaviziba vinywa vyao, na iseme Nasi mikono  yao , na itoe ushahidi miguu  yao kwa waliyokuwa wakiyachuma))  [Yaasiyn :65 ] Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya binaadamu aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "nimeiba".  Miguu itasema, "nimekwenda sehemu ya ma'asi". Macho yatasema, "nimetazama machafu".  Masikio yatasema, "nimesikiliza nyimbo, au umbea" na kadhalika. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Mola siku ya kufufuliwa,  watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya, Allaah  سبحانه وتعالى  Atawafunga midomo  yao na kuviamrisha viungo vizungumze:   عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى ال...